Salin ng mga Kahulugan ng Marangal na Qur'an - Salin sa Wikang Swahili ni Ali Mohsin Al-Barwani

Ad-Dukhan

external-link copy
1 : 44

حمٓ

H'a Mim . info

H'a Mim. Imeanzia Sura hii kwa baadhi ya harufi za kutamkwa kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kufungulia Sura nyingi kwa harufi kama hizi.

التفاسير:

external-link copy
2 : 44

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha! info

Mwenyezi Mungu anaapa kwa Qur'ani yenye kuweka wazi Dini ya Haki, yenye kuwabainishia watu yaliyo na maslaha ya dunia yao na Akhera yao, ili kujuulisha utukufu wa cheo chake.

التفاسير:

external-link copy
3 : 44

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ

Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji. info

Hakika Sisi tumeanza kuiteremsha Qur'ani katika usiku ulio jaa kheri, wenye baraka nyingi, kwani ni mwendo wetu kuonya kwa kuwatuma Mitume na kuteremsha Vitabu.

التفاسير:

external-link copy
4 : 44

فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ

Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima! info

Katika usiku huu wenye baraka hupambanuliwa baina ya mambo yote yenye hikima, na Qur'ani ndio kilele cha hikima, na ndio pambanuo baina ya kweli na uwongo. Na kwa hivyo ndio ikateremshwa katika usiku huo.

التفاسير:

external-link copy
5 : 44

أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ

Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma. info

Nakusudia kwa jambo hili, yaani jambo kuu lenye kutoka kwetu kama ilivyo kwisha pita hukumu ya mpango wetu. Kwani ni shani yetu kutuma Mitume kwa Vitabu ili kuwafikishia waja wetu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 44

رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. info

Kwa ajili ya rehema ya Mola wako Mlezi kwa waja wake, amewatuma Mitume kwa watu wawafikishie uwongofu wake, kwani hakika Yeye peke yake, ndiye Mwenye kusikia kila cha kusikiwa, Mwenye kujua kila cha kujuulikana.

التفاسير:

external-link copy
7 : 44

رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini. info

Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini na haki, na mnaifuata, na mnaamini kuwa hakika ndio Yeye Mwenye kuteremsha Qur'ani kuwa ni rehema na uwongofu.

التفاسير:

external-link copy
8 : 44

لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo. info

Hapana Mungu isipo kuwa Yeye anaye stahiki kuabudiwa, Yeye peke yake, Mwenye kuhuisha na kufisha. Na Yeye peke yake, ndiye aliye kuumbeni nyinyi na kawaumba baba zenu wa mwanzo.

التفاسير:

external-link copy
9 : 44

بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ يَلۡعَبُونَ

Lakini wao wanacheza katika shaka. info

Lakini makafiri wana shaka na ukweli huu, wamo wakifuata pumbao lao. Na huo ndio mtindo wa watu wa pumbao na michezo, sio mwendo wa watu wa ilimu na yakini.

التفاسير:

external-link copy
10 : 44

فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٖ مُّبِينٖ

Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri, info

Basi ewe Mtume! Ngojea ukame utapo wateremkia, wakasibiwa na kukonda na udhaifu wa kuona, ikawa mtu huwa anaona baina ya mbingu na ardhi moshi dhaahiri shaahiri, akawa anasikia mvumo wake wala hauoni.

التفاسير:

external-link copy
11 : 44

يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٞ

Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu! info

Moshi huu utawazunguka wale wanao kadhibisha walio sibiwa na ukame, watasema kwa wingi wa kitisho: Hii ni adhabu kali na chungu!

التفاسير:

external-link copy
12 : 44

رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ

Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. info

Kama pia watavyo sema kwa kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu: Hakika sisi tutaamini ukituondolea adhabu ya njaa na dhiki.

التفاسير:

external-link copy
13 : 44

أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مُّبِينٞ

Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha. info

Watu hawa watawaidhika vipi, hata watimize hiyo Imani wanayo iahidi wakiondolewa adhabu, na hali Mtume mwenye ujumbe ulio wazi kesha wajia na miujiza yenye kuonyesha ukweli wake, na hayo ndiyo mawaidha makubwa kabisa?

التفاسير:

external-link copy
14 : 44

ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٞ مَّجۡنُونٌ

Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu. info

Kisha wakaacha kumsadiki Mtume aliye tiliwa nguvu na miujiza iliyo wazi, na wakamwambia: Huo uwongo na uzushi! Mara nyengine wakimsingizia kuwa amefunzwa hayo na mtu, na mara nyengine kuwa akili yake imekorogeka.

التفاسير:

external-link copy
15 : 44

إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ

Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile! info

Mwenyezi Mungu anawarudi: Sisi hakika tutakuondoleeni adhabu wakati wa duniani, nao ni wakati mchache, lakini nyinyi mtarejea tu, bila ya shaka, yale yale mliyo kuwa mkiyatenda.

التفاسير:

external-link copy
16 : 44

يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ

Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa. info

Ewe Mtume! Watajie ile siku tutapo washika kwa mshiko mkubwa, wa nguvu. Nasi kwa mshiko huu ndio tunawatesa.

التفاسير:

external-link copy
17 : 44

۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ

Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu. info

Na bila ya shaka tulikwisha wafanyia mtihani, kabla ya makafiri wa Makka, kaumu ya Firauni kwa kuwaitia kwenye Imani, na akawajia Musa, Mtume Mtukufu kwa Mwenyezi Mungu. Wakamkataa kwa inda tu. Na huo ndio mtindo wa hawa washirikina.

التفاسير:

external-link copy
18 : 44

أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ

Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu. info

Mtume Mtukufu aliwaambia: Nipeni enyi waja wa Mwenyezi Mungu lilio waajibu juu yenu, nalo ni kuitikia wito wangu, kwani mimi ni Mtume nimetumwa makhsusi kwenu, na ni muaminifu katika ujumbe wangu.

التفاسير: