పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అలీ ముహ్సిన్ అల్ బర్వానీ

Al-Qalam

external-link copy
1 : 68

نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ

Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo! info

Nuun, ndio harufi ya N, iliyo anzia Sura hii ni kama kupinzana na hao wanao kadhibisha, na ili kuwazindua wenye kusadiki. Naapa kwa kalamu wanayo andikia Malaika na wenginewe, na hayo mambo ya kheri na manufaa wanayo yaandika,

التفاسير:

external-link copy
2 : 68

مَآ أَنتَ بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ بِمَجۡنُونٖ

Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. info

Hakika wewe, na Mwenyezi Mungu amekuneemesha kwa kukupa Unabii, si mchachefu wa akili, wala mpumbavu wa mawazo.

التفاسير:

external-link copy
3 : 68

وَإِنَّ لَكَ لَأَجۡرًا غَيۡرَ مَمۡنُونٖ

Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. info

Na hakika unapata thawabu kubwa zisio katika kwa ajili ya kufikisha Ujumbe.

التفاسير:

external-link copy
4 : 68

وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٖ

Na hakika wewe una tabia tukufu. info

Na hakika wewe bila ya shaka umeshikamana na sifa nzuri kabisa na vitendo vizuri kabisa alivyo kuumba navyo Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 68

فَسَتُبۡصِرُ وَيُبۡصِرُونَ

Karibu utaona, na wao wataona! info

Karibuni hivi, ewe Muhammad, utaona, na makafiri wataona,

التفاسير:

external-link copy
6 : 68

بِأَييِّكُمُ ٱلۡمَفۡتُونُ

Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. info

Ni nani kati yenu aliye mwenda wazimu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 68

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. info

Hakika Mola wako Mlezi, Yeye ndiye Mwenye kumjua zaidi aliye iacha Njia yake, na Yeye ndiye Mwenye kuwajua zaidi wenye akili walio ongoka kumwendea Yeye.

التفاسير:

external-link copy
8 : 68

فَلَا تُطِعِ ٱلۡمُكَذِّبِينَ

Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. info

Basi usiyaache uliyo nayo ya kuwapinga wanao kanusha.

التفاسير:

external-link copy
9 : 68

وَدُّواْ لَوۡ تُدۡهِنُ فَيُدۡهِنُونَ

Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. info

Wanatamani lau ungeli kuwa laini kwao katika baadhi ya mambo, ili na wao wawe laini kwako, kwa tamaa upate kurudishiana nao. (Neno lililo tumiwa hapo "Tud- hinu fayud-hinuun", maana yake khasa "Upake mafuta na wao wapake mafuta". Kiswahili husema: Kumpaka mtu mafuta kwa mgongo wa chupa. Yaani kumpa sifa za uwongo, kumfanyia unaafiki. Kwa Kiarabu ni "Mudaahana". Kupakana mafuta)

التفاسير:

external-link copy
10 : 68

وَلَا تُطِعۡ كُلَّ حَلَّافٖ مَّهِينٍ

Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, info

Wala usiache mwendo wako ulio nao kwenda kinyume na kila mwingi wa viapo, mtu wa kudharauliwa,

التفاسير:

external-link copy
11 : 68

هَمَّازٖ مَّشَّآءِۭ بِنَمِيمٖ

Mtapitapi apitae akifitini. info

Mtapitapi mwenye kueneza aibu za watu, mwenye kuwasengenya watu, kuwasema kwa siri, mwenye kutwaa maneno baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi,

التفاسير:

external-link copy
12 : 68

مَّنَّاعٖ لِّلۡخَيۡرِ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, info

Mwingi wa kupinga kila la kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,

التفاسير:

external-link copy
13 : 68

عُتُلِّۭ بَعۡدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ

Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. info

Mgumu wa moyo, mwenye tabia ya ukavu, muovu maarufu kwa shari, juu ya sifa hizo mbovu alizo nazo.

التفاسير:

external-link copy
14 : 68

أَن كَانَ ذَا مَالٖ وَبَنِينَ

Ati kwa kuwa ana mali na watoto! info

Ati kwa kuwa anajiona yeye ana mali na watoto wengi! Amezikadhibisha Aya zetu na amezipuuza.

التفاسير:

external-link copy
15 : 68

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! info

Akisomewa Qur'ani husema: Hivi ni visa vya uwongo vya watu wa kale!

التفاسير:

external-link copy
16 : 68

سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلۡخُرۡطُومِ

Tutamtia kovu juu ya pua yake. info

Tutambandika alama juu ya pua yake ya kumganda, apate kufedheheka mbele za watu.

التفاسير:

external-link copy
17 : 68

إِنَّا بَلَوۡنَٰهُمۡ كَمَا بَلَوۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ إِذۡ أَقۡسَمُواْ لَيَصۡرِمُنَّهَا مُصۡبِحِينَ

Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. info

Sisi tumewafanyia mtihani watu wa Makka kwa kuwapa neema, nao wakazikufuru; kama tulivyo wafanyia mtihani hao watu wenye shamba, walipo chukua kiapo kuwa watakwenda vuna mazao ya shamba lao asubuhi mapema,

التفاسير:

external-link copy
18 : 68

وَلَا يَسۡتَثۡنُونَ

Wala hawakusema: Mungu akipenda! info

Wala wasimkumbuke Mwenyezi Mungu, wakafunganisha hilo jambo lao na kupenda kwake.

التفاسير:

external-link copy
19 : 68

فَطَافَ عَلَيۡهَا طَآئِفٞ مِّن رَّبِّكَ وَهُمۡ نَآئِمُونَ

Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! info

Basi ikaliteremkia shamba hilo balaa kubwa ilio toka kwa Mola wako Mlezi, na hali wao wamelala.

التفاسير:

external-link copy
20 : 68

فَأَصۡبَحَتۡ كَٱلصَّرِيمِ

Likawa kama usiku wa giza. info

Likawa hilo shamba kama usiku wa giza kwa masaibu yalio lifikia.

التفاسير:

external-link copy
21 : 68

فَتَنَادَوۡاْ مُصۡبِحِينَ

Asubuhi wakaitana. info

Asubuhi wakawa wanaitana:

التفاسير:

external-link copy
22 : 68

أَنِ ٱغۡدُواْ عَلَىٰ حَرۡثِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰرِمِينَ

Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. info

Amkeni mapema mwende kondeni kwenu kama mmeazimia kuvuna.

التفاسير:

external-link copy
23 : 68

فَٱنطَلَقُواْ وَهُمۡ يَتَخَٰفَتُونَ

Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, info

Wakatoka, nao wakinong'ona kuambizana:

التفاسير:

external-link copy
24 : 68

أَن لَّا يَدۡخُلَنَّهَا ٱلۡيَوۡمَ عَلَيۡكُم مِّسۡكِينٞ

Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. info

Msimwachie masikini yeyote kukuingilieni leo!

التفاسير:

external-link copy
25 : 68

وَغَدَوۡاْ عَلَىٰ حَرۡدٖ قَٰدِرِينَ

Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. info

Wakenda hapo asubuhi mpaka kwenye shamba lao, na azma yao ovu hiyo, na wao ni wenye uwezo kaamili wa kutenda hayo kwa kujigamba kwao.

التفاسير:

external-link copy
26 : 68

فَلَمَّا رَأَوۡهَا قَالُوٓاْ إِنَّا لَضَآلُّونَ

Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! info

Walipo liona limekuwa jeusi limeungua, walisema nao wamebabaika: Hakika sisi bila ya shaka tumepotea. Hili silo shamba letu!

التفاسير:

external-link copy
27 : 68

بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ

Bali tumenyimwa! info

Bali ndilo shamba letu! Na sisi tumenyimwa!

التفاسير:

external-link copy
28 : 68

قَالَ أَوۡسَطُهُمۡ أَلَمۡ أَقُل لَّكُمۡ لَوۡلَا تُسَبِّحُونَ

Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? info

Alisema aliye kuwa muadilifu wao na mbora wao akiwalaumu: Sikukwambieni mlipo kuwa mnasemezana kuwanyima masikini, hebu hamumkumbuki Mwenyezi Mungu mkaiacha niya yenu?

التفاسير:

external-link copy
29 : 68

قَالُواْ سُبۡحَٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. info

Wakasema walipo rejea kwenye uwongozi wao: Tunamtakasa Mwenyezi Mungu kuwa katudhulumu kwa yaliyo tusibu. Hakika sisi wenyewe ndio tumejidhulumu kwa makusudio yetu maovu.

التفاسير:

external-link copy
30 : 68

فَأَقۡبَلَ بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ يَتَلَٰوَمُونَ

Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. info

Wakawa wanaelekeana wao kwa wao wakilaumiana,

التفاسير:

external-link copy
31 : 68

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَٰغِينَ

Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! info

Wakisema: Huku ni kuhiliki kwetu! Hakika sisi tulikuwa tumepita mipaka katika dhulma zetu.

التفاسير:

external-link copy
32 : 68

عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبۡدِلَنَا خَيۡرٗا مِّنۡهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ

Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. info

Asaa Mola wetu Mlezi akatupa badala lilio bora kuliko hili shamba letu. Hakika sisi tunamtaka Mola wetu Mlezi peke yake atupe msamaha na malipo.

التفاسير:

external-link copy
33 : 68

كَذَٰلِكَ ٱلۡعَذَابُۖ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ

Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! info

Mfano wa kama hayo yaliyo yasibu hilo shamba ndio inakuwa adhabu yangu ninayo iteremsha duniani kwa anaye stahiki. Na bila ya shaka adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi lau kuwa watu wanajua hayo.

التفاسير:

external-link copy
34 : 68

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمۡ جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. info

Hakika wachamngu watapata kwa Mola wao Mlezi Bustani za neema safi.

التفاسير:

external-link copy
35 : 68

أَفَنَجۡعَلُ ٱلۡمُسۡلِمِينَ كَٱلۡمُجۡرِمِينَ

Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? info

Je! Sisi tudhulumu katika hukumu yetu, tuwafanye Waislamu sawa na makafiri?

التفاسير:

external-link copy
36 : 68

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Mna nini? Mnahukumu vipi? info

Vipi mnahukumia mfano wa hukumu kama hii ya dhulma?

التفاسير:

external-link copy
37 : 68

أَمۡ لَكُمۡ كِتَٰبٞ فِيهِ تَدۡرُسُونَ

Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? info

Kwani mnacho kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu mnacho kisoma,

التفاسير:

external-link copy
38 : 68

إِنَّ لَكُمۡ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ

Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? info

Na humo yamo hayo mnayo yapenda?

التفاسير:

external-link copy
39 : 68

أَمۡ لَكُمۡ أَيۡمَٰنٌ عَلَيۡنَا بَٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّ لَكُمۡ لَمَا تَحۡكُمُونَ

Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? info

Au kwani mnazo ahadi juu yetu zenye kutiliwa mkazo kwa viapo, zenye kubaki mpaka Siku ya Kiyama, kwamba mnayo haki ya hayo mnayo jihukumia?

التفاسير:

external-link copy
40 : 68

سَلۡهُمۡ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ

Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? info

Ewe Muhammad! Waulize washirikina: Ni nani dhamini wa hukumu hiyo?

التفاسير:

external-link copy
41 : 68

أَمۡ لَهُمۡ شُرَكَآءُ فَلۡيَأۡتُواْ بِشُرَكَآئِهِمۡ إِن كَانُواْ صَٰدِقِينَ

Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. info

Kwani wanao wanao shirikiana nao, na wanao fuata mwendo wao katika kauli yao hii? Basi na wawalete hao washirika wao, ikiwa wao ni wasema kweli katika madai yao.

التفاسير:

external-link copy
42 : 68

يَوۡمَ يُكۡشَفُ عَن سَاقٖ وَيُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ

Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, info

Siku mambo yatapo shitadi na yakawa magumu, na wakatakiwa makafiri wasujudu kwa kuwaemea na kuwakejeli, na wasiweze, (Kuwekwa wazi mundi, ni kinaya ya kudhihirishwa kweli yote Siku ya kwima kondo, Siku ya Kiyama. Chambilecho Sayyid Abdulla bin Ali bin Nassir katika Al Inkishaf: Tafakari siku ya kwima kondo Ya kuaridhiwa kila kitendo Pindi madhulumu atapo ondo Achamba Ya Rabi namua naye)

التفاسير:

external-link copy
43 : 68

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۖ وَقَدۡ كَانُواْ يُدۡعَوۡنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمۡ سَٰلِمُونَ

Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima info

Macho yao yameinama chini, yamefunikwa na fedheha. Na duniani walikuwa wakitakiwa wasujudu walipo kuwa wakiweza na wakakataa kusujudu.

التفاسير:

external-link copy
44 : 68

فَذَرۡنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِۖ سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ

Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. info

Ewe Muhammad! Nachilie na hao wanao ikadhibisha Qur'ani. Tutawajongeza kwenye adhabu kidogo kidogo kwa jiha wasio ijua kuwa adhabu itatokea huko.

التفاسير:

external-link copy
45 : 68

وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ

Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. info

Na nitawapa muhula kwa kuiakharisha adhabu. Hakika mipango yangu ni ya nguvu, na hawezi kuporonyoka yeyote akasalimika nayo.

التفاسير:

external-link copy
46 : 68

أَمۡ تَسۡـَٔلُهُمۡ أَجۡرٗا فَهُم مِّن مَّغۡرَمٖ مُّثۡقَلُونَ

Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? info

Kwani wewe unawaomba ujira kwa kuufikisha Ujumbe wako, na kwa hivyo wao wanaona uzito kwa gharama hiyo unayo wakalifisha?

التفاسير:

external-link copy
47 : 68

أَمۡ عِندَهُمُ ٱلۡغَيۡبُ فَهُمۡ يَكۡتُبُونَ

Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? info

Au kwani wao wanajua yaliyo fichikana na wao wanayaandika na ndio wanahukumu kwa hayo?

التفاسير:

external-link copy
48 : 68

فَٱصۡبِرۡ لِحُكۡمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلۡحُوتِ إِذۡ نَادَىٰ وَهُوَ مَكۡظُومٞ

Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. info

Basi wewe subiri kwa tunavyo wapa muhula na kukuakhirisha kukuletea manusura yetu juu yao. Wala usiwe kama Yunus, aliye mezwa na samaki, akawa na haraka na kuwaghadhibikia watu wake, alipo mnadia Mola wake Mlezi, naye kajaa hasira na ghadhabu, akitaka waadhibiwe kwa haraka.

التفاسير:

external-link copy
49 : 68

لَّوۡلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعۡمَةٞ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلۡعَرَآءِ وَهُوَ مَذۡمُومٞ

Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. info

Lau kuwa neema ya Mola wake Mlezi haikumdiriki kwa kukubali toba yake, angeli tupwa kutokana na tumbo la samaki ufukweni, naye akiteseka kwa kuteleza kwake.

التفاسير:

external-link copy
50 : 68

فَٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. info

Lakini Mola wake Mlezi kamteuwa kwa kuikubali toba yake, na akamjaalia miongoni mwa watu wema.

التفاسير:

external-link copy
51 : 68

وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَيُزۡلِقُونَكَ بِأَبۡصَٰرِهِمۡ لَمَّا سَمِعُواْ ٱلذِّكۡرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجۡنُونٞ

Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. info

Na makafiri wangeli karibia kukutelezesha na pahala pako, kwa jicho lao wanalo kuangalia kwa uadui na chuki wanapo isikia Qur'ani, wakisema: Hakika huyu ni mwendawazimu.

التفاسير:

external-link copy
52 : 68

وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. info

Na Qur'ani si chochote ila ni mawaidha, na hikima, na ukumbusho kwa walimwengu wote.

التفاسير: