పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అలీ ముహ్సిన్ అల్ బర్వానీ

Yusuf

external-link copy
1 : 12

الٓرۚ تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. info

Alif, Lam, Raa. Hizi harufi na mfano wake, zinazo fanya maneno yenu, enyi Waarabu, ndizo hizo hizo zinazo fanya Aya za hichi Kitabu, ambacho ni muujiza unao waemea watu kuuiga. Muujiza ulio wazi unao fafanua kwa kila mwenye kutafuta uwongozi ndani yake, na uwongofu. Na kwa hizi harufi za kutamkika zikasikilizana sauti yake wanazinduliwa watu watanabahi. Basi wasikilize, ijapo kuwa waliwafikiana kuwa wasisikilize.

التفاسير:

external-link copy
2 : 12

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia. info

Hakika Sisi tumemteremshia Mtume wetu haya maneno kwa lugha yenu ya Kiarabu yasomwe na yahifadhiwe, ili muyafahamu, na muwafikishie watu wote.

التفاسير:

external-link copy
3 : 12

نَحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ أَحۡسَنَ ٱلۡقَصَصِ بِمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ هَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبۡلِهِۦ لَمِنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ

Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua. info

Sisi tunakusimulia, ewe Nabii, visa vizuri kabisa kwa kukufunulia Kitabu hichi. Na kabla ya haya ulikuwa umeghafilika nayo, huyajui, haya, wala mawaidha yaliomo ndani yake, na Aya zake zilizo wazi.

التفاسير:

external-link copy
4 : 12

إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ إِنِّي رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُهُمۡ لِي سَٰجِدِينَ

Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia. info

Katika visa hivi, ewe Nabii, kipo hichi kisa cha Yusuf, pale alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeona usingizini nyota hidaa'shara, (kumi na moja) na jua, na mwezi. Nimeona vyote hivyo vikininyenyekea, vikisujudu mbele yangu. Yusuf, Alayhi Ssalam, alikuwa mwana wa Yaaqub, Muabrani, Mkanaani. Akauzwa Misri katika enzi ya utawala wa wavamizi wa kigeni waitwao Wahiksos. Na kwa ionekanavyo hao Wahiksos ni katika kabila za Kisami walio ingia Misri kutoka Sham wakaiteka Delta ya Misri mnamo mwaka 1730 k.k. ( kabla ya Nabii Isa a.s.) na kabla ya kumalizika enzi ya ukoo wa kumi na tatu wa Mafirauni. Wakaihukumu Misri kwa muda wa karne unusu. Wakafukuzwa mnamo mwaka 1580 k.k. na Ahmas wa Mwanzo aliye anzisha ukoo wa 18. Wakatolewa nje ya mipaka ya Misri.

التفاسير: