పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అబ్దుల్లాహ్ ముహమ్మద్ మరియు నాసర్ ఖమీస్

పేజీ నెంబరు:close

external-link copy
96 : 19

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَيَجۡعَلُ لَهُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وُدّٗا

Hakika wale waliomuamini Mwenyezi Mungu, wakawafuata Mitume Wake na wakatenda mema kulingana na sheria Yake, Mwingi wa rehema Atatia katika nyoyo za waja Wake mahaba ya kuwapenda. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 19

فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ ٱلۡمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِۦ قَوۡمٗا لُّدّٗا

Hakika sisi tumeirahisisha hii Qur’ani katika ulimi wako wa Kiarabu, ewe Mtume, ili uwape bishara wachamungu, miongoni mwa wafuasi wako, na uwaonye kwayo wakanushaji wenye utesi sana kwa njia isiyofaa. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 19

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هَلۡ تُحِسُّ مِنۡهُم مِّنۡ أَحَدٍ أَوۡ تَسۡمَعُ لَهُمۡ رِكۡزَۢا

Na mara nyingi tumewaangamiza ummah waliotangulia kabla ya watu wako, humuoni yoyote miongoni mwao na husikii sauti yao, basi hivyo ndivyo watakavyokuwa makafiri wa watu wako, tutawaangamiza kama tulivyowaangamiza waliotanguli kabla yao. Katika hii pana onyo na agizo la kuwaangamiza wakanushaji wenye ushindani wa ubatilifu. info
التفاسير: