పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అబ్దుల్లాహ్ ముహమ్మద్ మరియు నాసర్ ఖమీస్

పేజీ నెంబరు:close

external-link copy
65 : 19

رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَٰدَتِهِۦۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُۥ سَمِيّٗا

«Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.» info
التفاسير:

external-link copy
66 : 19

وَيَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَءِذَا مَا مِتُّ لَسَوۡفَ أُخۡرَجُ حَيًّا

Na binadamu kafiri anasema, kwa kukanusha kufufuliwa baada ya kufa, «Je mimi nikifa na nikamalizika, kweli nitatolewa kwenye kaburi langu nikiwa hai?» info
التفاسير:

external-link copy
67 : 19

أَوَلَا يَذۡكُرُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ وَلَمۡ يَكُ شَيۡـٔٗا

Vipi binadamu huyu kafiri amejisahau nafsi yake? Kwani hakumbuki kwamba sisi tulimuumba mara ya kwanza na hakuwa ni kitu kilichoko? info
التفاسير:

external-link copy
68 : 19

فَوَرَبِّكَ لَنَحۡشُرَنَّهُمۡ وَٱلشَّيَٰطِينَ ثُمَّ لَنُحۡضِرَنَّهُمۡ حَوۡلَ جَهَنَّمَ جِثِيّٗا

Naapa kwa Mola wako, ewe Muhammad, tutawakusanya hawa wenye kukanusha kufufuliwa Siku ya Kiyama pamoja na Mashetani, kisha tutawaleta wote kando ya moto wa Jahanamu wakiwa wamepiga magoti, kwa ukubwa wa misukosuko ambayo wamo ndani yake, hali ya kuwa hawawezi kusimama. info
التفاسير:

external-link copy
69 : 19

ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمۡ أَشَدُّ عَلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ عِتِيّٗا

Kisha tutawachukua, katika kila pote, wale wakiukaji amri zaidi na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu zaidi, tuanze kuwaadhibu. info
التفاسير:

external-link copy
70 : 19

ثُمَّ لَنَحۡنُ أَعۡلَمُ بِٱلَّذِينَ هُمۡ أَوۡلَىٰ بِهَا صِلِيّٗا

Kisha sisi ni tunawajua zaidi wale wanaostahili kuingia Motoni na kuadhibika kwa joto lake. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 19

وَإِن مِّنكُمۡ إِلَّا وَارِدُهَاۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتۡمٗا مَّقۡضِيّٗا

Na hakuna katika nyinyi, enyi watu, yoyote isipokuwa ataufikia huo Moto kwa kupita juu Ṣirāṭ (Njia) iliyotandikwa juu ya daraja la moto wa Jahanamu, kila mmoja kulingana na matendo yake. Hilo ni jambo lenye kuwa kwa lazima, Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, Amepitisha na Ameamua kwamba halina budi kuwa, hakuna namana ya kuliepuka. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 19

ثُمَّ نُنَجِّي ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّنَذَرُ ٱلظَّٰلِمِينَ فِيهَا جِثِيّٗا

Kisha tutawaokoa wale ambao walimcha Mola wao kwa kumtii na kujiepusha na kumuasi na tuwaache Motoni wale waliojidhulumu nafsi zao katika hali ya kupiga magoti. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 19

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَيُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ خَيۡرٞ مَّقَامٗا وَأَحۡسَنُ نَدِيّٗا

Na watu wakisomewa aya zetu zilizoteremshwa zilizo wazi, wale waliomkanusha Mwenyezi Mungu wanasemakawaambia Waumini, «Ni pote gani kati yetu na nyinyi lenye mashukio bora zaidi na makalio mazuri zaidi?» info
التفاسير:

external-link copy
74 : 19

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَحۡسَنُ أَثَٰثٗا وَرِءۡيٗا

Na ni mara nyingi tumewaangamiza ummah kabla ya hawa watu wako, ewe Mtume, waliokuwa na vitu vingi kuliko walivyokuwa navyo watu wako na mandhari ya kupendeza zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
75 : 19

قُلۡ مَن كَانَ فِي ٱلضَّلَٰلَةِ فَلۡيَمۡدُدۡ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ مَدًّاۚ حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ إِمَّا ٱلۡعَذَابَ وَإِمَّا ٱلسَّاعَةَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ هُوَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضۡعَفُ جُندٗا

Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Aliyekuwa amepotea njia ya haki asiyeifuata njia ya uongofu, Mwenyezi Mungu Atampa muhula na Atamnyoshea katika ule upotevu wake, mpaka atakapoyaona kwa yakini yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu : ima adhabu ya haraka ulimwenguni au kusimama saa ya Kiyama, hapo atajuwa ni nani aliyopo na aliyetulia mahali pabaya na aliye mnyonge wa nguvu na askari. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 19

وَيَزِيدُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱهۡتَدَوۡاْ هُدٗىۗ وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابٗا وَخَيۡرٞ مَّرَدًّا

Na Mwenyezi Mungu Anawaongezea waja Wake, walioongoka katika dini Yake, uongofu juu ya uongofu walionao kwa yale yanayowapitia mara kwa mara ya kuyaamini malazimisho ya Mwenyezi Mungu na kuyafuata kivitendo. Na matendo mema yaliyosalia yana malipo bora kwa Mwenyezi Mungu kesho Akhera, na yana matokeo bora na mwisho mwema. info
التفاسير: