அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் bபிர்வானி

Az-Zukhruf

external-link copy
1 : 43

حمٓ

H'a Mim . info

H'a Mim:- Imeanza Sura hii kwa baadhi ya harufi za kutamkwa kama ilivyo ada ya Qur'ani katika kuanzishia Sura nyingi kwa harufi kama hizi.

التفاسير:

external-link copy
2 : 43

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha. info

Mwenyezi Mungu, Subhanahu, anaapa kwa Qur'ani inayo eleza wazi yale iliyo yakusanya katika mambo ya itikadi na hukumu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 43

إِنَّا جَعَلۡنَٰهُ قُرۡءَٰنًا عَرَبِيّٗا لَّعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ

Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu. info

Hakika Sisi tumeijaalia Qur'ani iwe kwa lugha ya Kiarabu, ili mweze kuelewa umuujiza wake, na mweze kuzingatia maana zake.

التفاسير:

external-link copy
4 : 43

وَإِنَّهُۥ فِيٓ أُمِّ ٱلۡكِتَٰبِ لَدَيۡنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ

Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye hikima. info

Na hakika hii Qur'ani iliyo thibiti katika Lauhun Mahfuudh, Ubao ulio hifadhiwa, ulioko kwetu, bila ya shaka, ina cheo cha juu, na imepangwa kwa mpango wa hikima, katika mwisho wa ufasihi. (Vitabu vyote vya mbinguni asili yake anayo Mwenyezi Mungu, katika Ujuzi wake wa tokea azali, Al- I'lmu al-azaliy au Ubao Ulio Hifadhiwa Al-lauhu al-mahfuudh au Asili ya Maandiko Ummu-l-kitabi. Kwa sababu ya kuwa Vitabu vilivyo kuja zamani, ikiwa Taurati, Zaburi, Injili n.k. vilikuwa ni vya muda fulani, na kwa mataifa fulani, basi haikuwepo dharura vibaki kwa usafi kila neno lake. Ni makusudio yake tu yabakie, yaliyo kuwa ya msingi. Ama ulipo fika wakati wa kudumisha Ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa zama zote, na kwa watu wote, ndio ikaja Qur'ani ambayo imehifadhiwa kila neno lake. Na ndio siri ya kuletwa kwa lugha ya Kiarabu na ikalindwa kwa lugha ile, ijapo kuwa itatarajumiwa katika lugha nyengine. Mzozano wowote unao tokea unarejezwa kwenye asli ile ya Kiarabu ambayo haikubadilika hata chembe, wala haitabadilika mpaka Siku ya Kiyama. Huo peke yake ni muujiza. Ama vitabu vya Biblia ni kama maji yaliyo tibuliwa na ng'ombe mpaka kwenye chemchem yake. Chemchem ya Qur'ani haikutibuliwa. Ijapo kuwa wanyama na watu wanaweza kunywa maji yake huku chini, kwenye kitovu cha chemchem hakuguswi. Huko ni kwenye Qur'ani hiyo ya Kiarabu, safi kama ilivyo kwenye Ubao Ulio Hifadhiwa.)

التفاسير:

external-link copy
5 : 43

أَفَنَضۡرِبُ عَنكُمُ ٱلذِّكۡرَ صَفۡحًا أَن كُنتُمۡ قَوۡمٗا مُّسۡرِفِينَ

Je! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa ukafiri? info

Je! Tukupeni muhula, tuache kukuteremshieni Qur'ani kwa kukutupilieni mbali, kwa sababu ya kupita kwenu mipaka ya ukafiri juu ya nafsi zenu? Hayawi hayo, kwa kufuata hukumu ya kulazimikana kwenu na hoja.

التفاسير:

external-link copy
6 : 43

وَكَمۡ أَرۡسَلۡنَا مِن نَّبِيّٖ فِي ٱلۡأَوَّلِينَ

Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani! info

Nasi tuliwatuma Manabii wengi kuyaendea mataifa yaliyo tangulia, basi hapana ajabu kitu kumtuma Mtume kwenu.

التفاسير:

external-link copy
7 : 43

وَمَا يَأۡتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli. info

Wala hawajii Mtume yeyote kuwakumbusha Haki ila huendelea na kumfanyia maskhara.

التفاسير:

external-link copy
8 : 43

فَأَهۡلَكۡنَآ أَشَدَّ مِنۡهُم بَطۡشٗا وَمَضَىٰ مَثَلُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Na tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita. info

Basi tuliwateketeza walio kadhibisha walio tangulia; na hao walikuwa wamewazidi makafiri wa Makka kwa nguvu na ushupavu. Basi wasidanganyike hawa na ujabari wao. Na zilikwisha tangulia katika Qur'ani hadithi za ajabu za watu wa kale, za kuwafanya wenginewe wazingatie. Basi enyi mnao kanusha! Zingatieni!

التفاسير:

external-link copy
9 : 43

وَلَئِن سَأَلۡتَهُم مَّنۡ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡعَلِيمُ

Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi! info

Na ninaapa, ewe Mtume! Ukiwauliza makafiri nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema kuyajibu hayo: Mwenyezi Mungu ndiye aliye ziumba, ambaye anasifika kwa hakika ya mambo kuwa ni Mwenye nguvu, na Mwenye Ujuzi ulio enea.

التفاسير:

external-link copy
10 : 43

ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مَهۡدٗا وَجَعَلَ لَكُمۡ فِيهَا سُبُلٗا لَّعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ

Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate kuongoka. info

Ambaye amekufanyieni ardhi ni pahala palipo tanda, ili muweze kukaa humo na mjitumilie, na akakufanyieni ndani yake njia mnazo zipitia katika safari zenu mpate kufikia mtakako.

التفاسير: