அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு - அப்துல்லா முஹம்மது மற்றும் நாசர் காமிஸ்

பக்க எண்:close

external-link copy
118 : 11

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخۡتَلِفِينَ

Na lau Mola wako Alitaka, Angaliwafanya watu wote ni kundi moja, wako kwenye dini moja , nayo ni dini ya Uislamu. Lakini Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, hakutaka hivyo. Basi watu hawataacha kuendelea kutafautiana katika dini zao, na hayo ndiyo yanayoambatana na hekima Yake. info
التفاسير:

external-link copy
119 : 11

إِلَّا مَن رَّحِمَ رَبُّكَۚ وَلِذَٰلِكَ خَلَقَهُمۡۗ وَتَمَّتۡ كَلِمَةُ رَبِّكَ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ أَجۡمَعِينَ

Isipokuwa wale waliorehemewa na Mola wako, wakamuamini Yeye na wakawafuata Mitume Wake, kwani wao hawatafautiani juu ya kumpwkwesha Mwenyezi Mungu na yale ambayo Mitume wamekuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Ni matakwa ya Hekima Yake, Aliyetakata na sifa za upungufu na Akatukuka, kwamba Yeye Amewaumba wao wakiwa wametafautiana: kuna kundi ovu na kundi lema; na kila kundi limesahilishiwa kwa lile lililoumbiwa, na kwa hii ndipo agizo la Mwenyezi Mungu litatimia la kuwa Yeye Ataujaza, Moto wa Jahanamu, majini na binadamu waliomfuata Iblisi na askari wake na wasiongoke kwenye njia ya Imani. info
التفاسير:

external-link copy
120 : 11

وَكُلّٗا نَّقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَۚ وَجَآءَكَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَقُّ وَمَوۡعِظَةٞ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Na tunakupa habari, ewe Mtume, za Mitume waliokuwa kabla yako zenye kila unalohitajia la kuupa nguvu moyo wako ya kusimama imara ili kubeba majukumu ya Utume. Na umekujia wewe, katika sura hii na hahabri zilizomo, ufafanuzi wa haki ambayo wewe uko juu yake. Na yamekujia wewe, katika hii sura, mawaidha ya kuwafanya makafiri wakomeke na ukumbusho wa kuwafanya wenye kumuamini Mwenyezi mungu na Mitume Wake wakumbuke. info
التفاسير:

external-link copy
121 : 11

وَقُل لِّلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ ٱعۡمَلُواْ عَلَىٰ مَكَانَتِكُمۡ إِنَّا عَٰمِلُونَ

Waambie, ewe Mtume, makafiri wasiokubali upweke wa Mwenyezi Mungu, «Fanyeni mnayoyafanya kwa namna yenu na mbinu zenu za kuupinga Ulinganizi na kumkera Mtume na wale waliomuitika, kwani sisi ni wenye kufanya kwa namna yetu mbinu zetu za kusimama imara juu ya Dini yetu na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
122 : 11

وَٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ

Na ungojeni mwisho wa jambo letu, na sisi tunangojea mwisho wa jambo lenu.» Katika hii pana onyo na kitisho kwao. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 11

وَلِلَّهِ غَيۡبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ يُرۡجَعُ ٱلۡأَمۡرُ كُلُّهُۥ فَٱعۡبُدۡهُ وَتَوَكَّلۡ عَلَيۡهِۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ

Ni wa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, ujuzi wa kila kisichoonekana mbinguni na ardhini. Na Kwake yanarejeshwa mambo yote Siku ya Kiyama. Basi muabudu Yeye, ewe Nabii, na umtegemezee mambo yako Kwake. Na Mola wako Hakuwa ni mwenye kughafilika na yale mnayoyafanya ya wema na uovu na Atamlipa kila mtu kwa matendo yake. info
التفاسير: