அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு - அப்துல்லா முஹம்மது மற்றும் நாசர் காமிஸ்

பக்க எண்:close

external-link copy
98 : 11

يَقۡدُمُ قَوۡمَهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فَأَوۡرَدَهُمُ ٱلنَّارَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡوِرۡدُ ٱلۡمَوۡرُودُ

Fir'awn atatangulia akiwaongoza watu wake Siku ya Kiyama mpaka awatie Motoni. Ni mahali pabaya ambapo wao wataiangia. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 11

وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِۦ لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ بِئۡسَ ٱلرِّفۡدُ ٱلۡمَرۡفُودُ

Na Mwenyezi Mungu Amewafuatishia laana katika ulimwengu huu, pamoja na adhabu Aliyowaharakishia ya kuzamishwa baharini. Na Siku ya Kiyama pia atawapa laana nyingine kwa kuwatia Motoni. Ni mabaya sana mambo yaliyokusanyika kwao na yakafuatana juu yao, ya adhabu ya Mwenyezi Mungu na laana ya duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 11

ذَٰلِكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّهُۥ عَلَيۡكَۖ مِنۡهَا قَآئِمٞ وَحَصِيدٞ

Haya tuliyokutajia wewe, ewe Mtume, ni miongoni mwa habari za watu wa miji ambayo tuliwaangamiza watu wake, twakupasha habari zake. Na miongoni mwa miji hiyo kuna iliyo na athari zilizosalia; na miongoni mwazo kuna ambazo athari zake zimefutika, hakuna chochote katika hizo kilichosalia. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 11

وَمَا ظَلَمۡنَٰهُمۡ وَلَٰكِن ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡۖ فَمَآ أَغۡنَتۡ عَنۡهُمۡ ءَالِهَتُهُمُ ٱلَّتِي يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ لَّمَّا جَآءَ أَمۡرُ رَبِّكَۖ وَمَا زَادُوهُمۡ غَيۡرَ تَتۡبِيبٖ

Hakukuwa kuwaangamiza wao ni bila ya sababu na dhambi zinazowafanya wastahili hayo, lakini walijidhulumu wenyewe kwa ushirikina wao na kuleta kwao uharibifu katika ardhi. Hawakuwapa nafuu wao hao waungu wao ambao walikuwa wakidai kuwa ni waungu na wakiwataka wawaondolee shida, wakati amri ya Mwenyezi Mungu ilipokuja ya kuwaadhibu wao. Na hao waungu wao hawakuwazidishia isipokuwa uvunjaji, maangamivu na hasara. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 11

وَكَذَٰلِكَ أَخۡذُ رَبِّكَ إِذَآ أَخَذَ ٱلۡقُرَىٰ وَهِيَ ظَٰلِمَةٌۚ إِنَّ أَخۡذَهُۥٓ أَلِيمٞ شَدِيدٌ

Na kama nilivyowapatiliza kwa adhabu watu wa miji iliyodhulumu kwa kuenda kinyume na amri yangu na kuwakanusha Mitume wangu, nitawapatiliza wengineo miongoni mwa watu wa miji wakizidhulumu nafsi zao kwa kumkanusha Mwenyezi Mungu na kumuasi Yeye na kuwakanusha Mitume Wake. Hakika mapatilizo Yake ya mateso ni makali, yenye kuumiza, yaliyo magumu. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 11

إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّمَنۡ خَافَ عَذَابَ ٱلۡأٓخِرَةِۚ ذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّجۡمُوعٞ لَّهُ ٱلنَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوۡمٞ مَّشۡهُودٞ

Hakika katika kuwapatiliza watu wa miji iliyotangulia iliyodhulumu, ni mazingatio na mawaidha kwa anayeogopa mateso ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake huko Akhea. Siku hiyo ni ambayo watakusanywa watu wote ili wahesabiwe na walipwe, na wataishuhudia viumbe wote. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 11

وَمَا نُؤَخِّرُهُۥٓ إِلَّا لِأَجَلٖ مَّعۡدُودٖ

Na hatuicheleweshi Siku ya Kiyama isipokuwa ni ukome muda uliyohesabiwa uliyo kwenye elimu yetu, hauzidi wala haupungui na kipimo chetu tulichoupimia kwa hekima yetu. info
التفاسير:

external-link copy
105 : 11

يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ

Siku kitakapokuja Kiyama, hakuna nafsi itakayosema isipokuwa kwa idhini ya Mola Wake. Kati yao kuna shaqiyy (muovu) anayestahili adhabu na kuna sa'īd (mwema) aliyefadhiliwa kwa kupewa starehe. info
التفاسير:

external-link copy
106 : 11

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ شَقُواْ فَفِي ٱلنَّارِ لَهُمۡ فِيهَا زَفِيرٞ وَشَهِيقٌ

Ama wale waliokuwa waovu ulimwenguni kwa kuharibika akida yao na uovu wa vitendo vyao, basi Moto utakuwa ndio mahali pao pa kutulia; humo watakuwa na kutoa pumzi kutoka kwenye vifua kwa nguvu na kurudisha kwa shida, na sauti mbili hizo ni mbaya zaidi zilizopita kiasi. info
التفاسير:

external-link copy
107 : 11

خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Watakuwa ni wenye kukaa humo milele muda wa kuweko mbingu na ardhi, hivyo basi adhabu yao haitakatika wala haitakoma, bali ni adhabu ya daima iliyotiliwa mkazo, isipokuwa iwapo Mola wako atataka, kwa kuwatoa waliompwekesha waliofanya maasia baada ya muda fulani wa kukaa kwao Motoni. Hakika Mola wako ni Mwenye kufanya Analolitaka. info
التفاسير:

external-link copy
108 : 11

۞ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ سُعِدُواْ فَفِي ٱلۡجَنَّةِ خَٰلِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلۡأَرۡضُ إِلَّا مَا شَآءَ رَبُّكَۖ عَطَآءً غَيۡرَ مَجۡذُوذٖ

Na ama wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaruzuku wema, wataingia Peponi wakae milele humo muda wa kuwako mbingu na ardhi, isipokuwa lile kundi ambalo Mwenyezi Mungu Atataka kulichelewesha, nalo ni lile la waliompwekesha Mwenyezi Mungu waliofanya maasia. Wao watasalia Motoni kwa kipindi fulani, kisha watatoka humo kwenda Peponi kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake. Na Mwenyezi Mungu Atawapa watu wema hawa vipaji visizopunguzwa. info
التفاسير: