ශුද්ධවූ අල් කුර්ආන් අර්ථ කථනය - ස්වහීලී පරිවර්තනය - අලි මුහ්සන් අල්බර්වානි

external-link copy
58 : 9

وَمِنۡهُم مَّن يَلۡمِزُكَ فِي ٱلصَّدَقَٰتِ فَإِنۡ أُعۡطُواْ مِنۡهَا رَضُواْ وَإِن لَّمۡ يُعۡطَوۡاْ مِنۡهَآ إِذَا هُمۡ يَسۡخَطُونَ

Na miongoni mwao wapo wanao kusengenya katika kugawa sadaka. Wanapo pewa wao huridhika. Na wakito pewa hukasirika. info

Na baadhi ya hawa wanaafiki wanakusema kwa ubaya, na wanakutia ila katika ugawaji wa sadaka na ngawira. Hawana ila uroho wa makombo ya kidunia tu. Ukiwapa wakitakacho wanakuwa radhi nawe kwa utendayo. Na kama hukuwapa ndio wao ni wepesi wa kukuletea maudhi.

التفاسير: