ශුද්ධවූ අල් කුර්ආන් අර්ථ කථනය - ස්වහීලී පරිවර්තනය - අබ්දුල්ලා මුහම්මද් සහ නාසර් ඛමීස්

Ash-Shams

external-link copy
1 : 91

وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَىٰهَا

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa jua na mchana wake na mwangaza wake wa asubuhi. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 91

وَٱلۡقَمَرِ إِذَا تَلَىٰهَا

Na kwa mwezi unapolifuata wakati wa kucha na kutwa. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 91

وَٱلنَّهَارِ إِذَا جَلَّىٰهَا

Na kwa mchana unapoliondoa giza na kulifunua. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 91

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰهَا

Na kwa usiku unapoifinika ardhi ikawa giza. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 91

وَٱلسَّمَآءِ وَمَا بَنَىٰهَا

Na kwa mbingu na kujengeka kwake kiimara. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 91

وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا طَحَىٰهَا

Na kwa ardhi na kutandikika kwake. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 91

وَنَفۡسٖ وَمَا سَوَّىٰهَا

Na kwa kila nafsi na namna Mwenyezi Mungu alivyoikamilisha umbo lake ili itekeleze kazi iliyoumbiwa nayo. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 91

فَأَلۡهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقۡوَىٰهَا

Akaibainishia njia ya shari na njia ya kheri. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 91

قَدۡ أَفۡلَحَ مَن زَكَّىٰهَا

Amefaulu mwenye kuisafisha na kuikuza kwa kheri. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 91

وَقَدۡ خَابَ مَن دَسَّىٰهَا

Na ameingia kwenye hasara mwenye kuitia nafsi yake kwenye maasia. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 91

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِطَغۡوَىٰهَآ

Kabila la Thamūd lilimkanusha Nabii wake kwa kuvama kwenye uasi. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 91

إِذِ ٱنۢبَعَثَ أَشۡقَىٰهَا

Pindi walipotoka wabaya zaidi wa kabila hilo kumchinja Ngamia. Mtume wa Mwenyezi Mungu’ Ṣāliḥ, amani imshukie, info
التفاسير:

external-link copy
13 : 91

فَقَالَ لَهُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ نَاقَةَ ٱللَّهِ وَسُقۡيَٰهَا

akawaambia: «Tahadharini kumgusa kwa ubaya ngamia ambaye ni miujiza ilioletwa na Mwenyezi Mungu kwenu inayoonyesha ukweli wa Nabii wenu, na msizuie kinywaji chake. Yeye ana siku yake ya kunywa na nyinyi mna siku yenu maalumu ya kunywa.» Hilo likawa zito kwao. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 91

فَكَذَّبُوهُ فَعَقَرُوهَا فَدَمۡدَمَ عَلَيۡهِمۡ رَبُّهُم بِذَنۢبِهِمۡ فَسَوَّىٰهَا

Wakamkanusha na kulipuza onyo lake wakamchinja.Mola wao Akawafinika kwa adhabu, akaisawazisha juu yao na hakuna aliyeweza kuponyoka. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 91

وَلَا يَخَافُ عُقۡبَٰهَا

Wala Haogopi, Mwenye uwezo uliotukuka, athari ya adhabu kali Aliywateremshia. info
التفاسير: