ශුද්ධවූ අල් කුර්ආන් අර්ථ කථනය - ස්වහීලී පරිවර්තනය - අබ්දුල්ලා මුහම්මද් සහ නාසර් ඛමීස්

පිටු අංක:close

external-link copy
13 : 67

وَأَسِرُّواْ قَوۡلَكُمۡ أَوِ ٱجۡهَرُواْ بِهِۦٓۖ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Na yaficheni maneno yenu, enyi watu, katika jambo lolote miongoni mwa mambo yenu , au yadhihirisheni, kwani yote mawili mbele ya Mwenyezi Mungu ni sawa. Hakika Yeye , kutakasika ni Kwake, ni Mjuzi wa yaliyomo ndani ya vifua, basi yatafichamana vipi maneno yenu na matendo yenu Kwake Yeye! info
التفاسير:

external-link copy
14 : 67

أَلَا يَعۡلَمُ مَنۡ خَلَقَ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلۡخَبِيرُ

Je, kwani hajui, Mola wa viumbe, viumbe Vyake na mambo yao na hali ni kuwa Yeye Ndiye Aliyewaumba, Akalitengeneza umbo lao na Akalifanya zuri? Na Yeye Ndiye Mpole kwa waja Wake, Ndiye Mwenye kuwatambua wao na matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 67

هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ ذَلُولٗا فَٱمۡشُواْ فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُواْ مِن رِّزۡقِهِۦۖ وَإِلَيۡهِ ٱلنُّشُورُ

Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Aliyewafanyia ardhi iwe nyepesi iliyotayarishwa mpate kutulia juu yake. Basi tembeeni sehemu zake na pande zake na mle riziki ya Mwenyezi Mungu Anayowatolea humo. Na Kwake Yeye Peke Yake ndio Ufufuzi kutoka makaburini mwenu ili mhesabiwe na mlipwe. Katika hii aya pana ishara ya kuhimiza utafutaji riziki na uchumaji. Pia pana dalili kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Muabudiwa wa haki Peke Yake Asiye na mshirika, na pana dalili ya uweza Wake, kukumbusha neema Zake na kuonya kuelemea duniani. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 67

ءَأَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يَخۡسِفَ بِكُمُ ٱلۡأَرۡضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ

Je mmesalimika, enyi makafiri wa Makkah, na Mwenyezi Mungu Aliye mbinguni kuwa Hatawadidimiza ardhini ikawa inatetemeka na nyinyi mpaka mkaangamia? info
التفاسير:

external-link copy
17 : 67

أَمۡ أَمِنتُم مَّن فِي ٱلسَّمَآءِ أَن يُرۡسِلَ عَلَيۡكُمۡ حَاصِبٗاۖ فَسَتَعۡلَمُونَ كَيۡفَ نَذِيرِ

Au mmesalimika kuwa Mwenyezi Mungu Aliye juu ya mbingu kuwa Hatawatumia upepo wenye kuwapiga mawe madogomadogo na hapo mkajua, enyi makafiri, ni vipi onyo langu kwenu mnapoiona adhabu? Na huko kujua wakati huo hakutawanufaisha. Katika hii aya pana kuthibitisha kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Yuko juu kwa namna inayonasibiana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 67

وَلَقَدۡ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ

Kwa hakika walikanusha wale waliokuwa kabla ya makafiri wa Makkah kama vile watu wa Nuchouh, 'Ād na Thamūd walivyowakanusha Mitume wao. Basi kulikuwa namna gani kule kuwakasirikia kwangu na kuwageuzia kwangu neema waliyokuwa nayo kwa kuwateremshia adhabu na kuwaangamiza? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 67

أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَى ٱلطَّيۡرِ فَوۡقَهُمۡ صَٰٓفَّٰتٖ وَيَقۡبِضۡنَۚ مَا يُمۡسِكُهُنَّ إِلَّا ٱلرَّحۡمَٰنُۚ إِنَّهُۥ بِكُلِّ شَيۡءِۭ بَصِيرٌ

Je kwani walighafilika hawa makafiri wasiwatazame ndege juu yao wakiwa wanazikunjua mbawa zao angani na wakati mwingine wanazikunja na kuzitia mbavuni mwao? Hakuna mwenye kuwatunza wasianguke wakiwa katika hali hiyo isipokuwa Mwingi wa rehema. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 67

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي هُوَ جُندٞ لَّكُمۡ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ ٱلرَّحۡمَٰنِۚ إِنِ ٱلۡكَٰفِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ

Hakika Yeye Anaona kila kitu, hakuna upungufu wala tofauti.Bali ni nani huyu ambaye, kulingana na madai yenu, enyi makafiri, kuwa ni kundi lenu, anayewanusuru asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, iwapo Yeye Atawatakia baya? Makafiri hawakuwa, katika madai yao isipokuwa wako katika kudanganywa na kupotezwa na Shetani. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 67

أَمَّنۡ هَٰذَا ٱلَّذِي يَرۡزُقُكُمۡ إِنۡ أَمۡسَكَ رِزۡقَهُۥۚ بَل لَّجُّواْ فِي عُتُوّٖ وَنُفُورٍ

Bali ni nani huyo mpaji anayedaiwa atakayewapa nyinyi riziki iwapo Yeye Atazuia riziki Yake na Atawakatalia kuwapa? Bali makafiri wanaendelea kwenye ukiukaji wao na upotevu wao wakiwa katika hali ya ushindani, kujiona na kuikimbia haki, hawaisikii wala hawaifuati. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 67

أَفَمَن يَمۡشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجۡهِهِۦٓ أَهۡدَىٰٓ أَمَّن يَمۡشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Je huyu anayetembea akiwa kichwa chake kimeinama hajui pa kuelekea wala namna ya kwenda yuko katika kulingana zaidi kwenye njia na ameongoka zaidi au ni yule anayetembea sawasawa, akiwa na kimo kilicholingana, aliye mzima, afuataye njia iliyofunuka wazi isiyokuwa na mpeteko? Na huu ni mfano Mwenyezi Mungu Amempigia kafiri na na Muumini. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 67

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَكُمۡ وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَٱلۡأَفۡـِٔدَةَۚ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ

Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewapatisha nyinyi kutoka kwenye hali ya kutokuwako, na akawafanya nyinyi muwe na mashikio ili msikie kwayo, macho ili muonee na nyoyo ili muelewe kwazo. Basi ni uchache, enyi makafiri, mnavyomtekelezea shukrani Mola wenu kwa neema hizi alizowaneemesha. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 67

قُلۡ هُوَ ٱلَّذِي ذَرَأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَإِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Waambie, «Mwenyezi Mungu ndiye Aliyewaumba na Akawaeneza ardhini. Na Kwake Yeye, PekeYake, mtakusanywa baada ya huku kutengana, ili mhesabiwe na mlipwe.» info
التفاسير:

external-link copy
25 : 67

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Na wanasema hao makafiri, «Ni lini itakapohakikika ahadi hii, ewe Muhammad? Tupeni habari ya kipindi chake, enyi Waumini, iwapo nyinyi ni wakweli katika yale mnayoyadai.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 67

قُلۡ إِنَّمَا ٱلۡعِلۡمُ عِندَ ٱللَّهِ وَإِنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٞ مُّبِينٞ

Waambie hao, ewe Mtume, «Hakika ujuzi wa kipindi cha kusimama Kiyama uko kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Anayehusika nacho. Na hakika si lingine ni kwamba mimi ni muonyaji kwenu, ninawaogopesha mwisho mbaya wa ukafiri wenu na ninawaeleza kile Alichoniamrisha Mwenyezi Mungu nikibainishe upeo wa kubainisha. info
التفاسير: