ශුද්ධවූ අල් කුර්ආන් අර්ථ කථනය - ස්වහීලී පරිවර්තනය - අබ්දුල්ලා මුහම්මද් සහ නාසර් ඛමීස්

පිටු අංක:close

external-link copy
62 : 18

فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَىٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدۡ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَٰذَا نَصَبٗا

Walipoondoka pale mahali walipomsahau samaki, na Mūsā akahisi njaa, alimwambia mtumishi wake, «tuletee chakula chetu cha mwanzo wa mchana, hakika tumechoka kwenye safari yetu hii.» info
التفاسير:

external-link copy
63 : 18

قَالَ أَرَءَيۡتَ إِذۡ أَوَيۡنَآ إِلَى ٱلصَّخۡرَةِ فَإِنِّي نَسِيتُ ٱلۡحُوتَ وَمَآ أَنسَىٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيۡطَٰنُ أَنۡ أَذۡكُرَهُۥۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُۥ فِي ٱلۡبَحۡرِ عَجَبٗا

Mtumishi wake akamwambia, «Unakumbuka tuliposhukia kwenye jiwe ambapo tulipumzika? Nilisahau kukwambia habari ya yule samaki, na hakuna aliyenisahaulisha isipokuwa ni Shetani. Na yule samaki, aliyekuwa mekufa, uhai umemrudia, akajirusha baharini na akajitolea njia ya kwendea, na mambo yake ni yenye kustaajabiwa. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 18

قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبۡغِۚ فَٱرۡتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصٗا

Mūsā akasema, «Yaliyotokea ndiyo ambayo tulikuwa tukiyataka, kwani hiyo ni alama yangu ya mahali pa mja mwema.» Hapo wakarudi wakizifuata alama za nyayo zao mpaka wakakoma kwenye jiwe. info
التفاسير:

external-link copy
65 : 18

فَوَجَدَا عَبۡدٗا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَٰهُ رَحۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمٗا

Wakamkuta mja mwema miongoni mwa waja wetu ambaye ni al-Khaḍir, amani imshukiye- naye ni Nabii, miongono mwa Manabii wa Mwenyezi Mungu, ambaye Mwenyezi Mungu Amemfisha, tuliyempa rehema kutoka kwetu na tukamfundisha elimu kubwa itokayo kwetu. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 18

قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰ هَلۡ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰٓ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمۡتَ رُشۡدٗا

Mūsā akamsalimia na akamwambia, «Je, utaniruhusu nikufuate, unifundishe elimu ambayo Mwenyezi Mungu Amekufudisha kadiri ya mimi kujiongoza nayo na kunufaika? info
التفاسير:

external-link copy
67 : 18

قَالَ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِيَ صَبۡرٗا

Al-Khiḍir akawmwambia, «Hakika wewe , ewe Mūsā, hutaweza kuvumilia kunifuata na kuwa na mimi. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 18

وَكَيۡفَ تَصۡبِرُ عَلَىٰ مَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ خُبۡرٗا

Na utakuwa na uvumilivu kwa nitakalolifanya miongoni mwa mambo yaliyofichika kwako ambayo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Alinifundisha. info
التفاسير:

external-link copy
69 : 18

قَالَ سَتَجِدُنِيٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ صَابِرٗا وَلَآ أَعۡصِي لَكَ أَمۡرٗا

Mūsā akamwambia, «Utanikuta, Mwenyezi Mungu Akitaka, ni mwenye kuvumilia kwa nitakayoyaona kwao, na sitaenda kinyume na amri yako yoyote utakayoniamrisha. info
التفاسير:

external-link copy
70 : 18

قَالَ فَإِنِ ٱتَّبَعۡتَنِي فَلَا تَسۡـَٔلۡنِي عَن شَيۡءٍ حَتَّىٰٓ أُحۡدِثَ لَكَ مِنۡهُ ذِكۡرٗا

Al-Khiḍr akakubali na akamwambia, «Ukifuatana na mimi usiniulize juu ya chochote usichokikubali mpaka nikupe maelezo yake yaliyofichika kwako bila ya wewe kuuliza.» info
التفاسير:

external-link copy
71 : 18

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِي ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَاۖ قَالَ أَخَرَقۡتَهَا لِتُغۡرِقَ أَهۡلَهَا لَقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔا إِمۡرٗا

Wakatoka kwenda kwenye ufuo wa pwani, ikawapita mashua, wakawataka wenyewe wapande na wao. Walipopanda Al-Khiḍr aliukoboa ubao kutoka kwenye mashua na akaitoboa tundu. Mūsā akamwambia,»Umeitoboa mashua ili uwazamishe wenyewe, na hali wao walituchukua bila malipo? Kwa hakika umefanya jambo baya.» info
التفاسير:

external-link copy
72 : 18

قَالَ أَلَمۡ أَقُلۡ إِنَّكَ لَن تَسۡتَطِيعَ مَعِيَ صَبۡرٗا

Al-Khiḍr akamwambia, «Nilisema tangu mwanzo, ‘Hakika wewe hutoweza kuvumilia kuandamana na mimi.’» info
التفاسير:

external-link copy
73 : 18

قَالَ لَا تُؤَاخِذۡنِي بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرۡهِقۡنِي مِنۡ أَمۡرِي عُسۡرٗا

Mūsā akasema akitoa udhuru, «usinichukulie kwa kusahau sharti yako juu yangu wala usinikalifishe mashaka ya kujifunza kwako, na amiliana na mimi kwa usahali na upole.» info
التفاسير:

external-link copy
74 : 18

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَٰمٗا فَقَتَلَهُۥ قَالَ أَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا زَكِيَّةَۢ بِغَيۡرِ نَفۡسٖ لَّقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـٔٗا نُّكۡرٗا

Al-Khiḍr akakubali udhuru wake. Kisha wakatoka mashuani, na walipokuwa wanatembea kwenye ufuo wa pwani, ghafla wakamuona mvulana yuwacheza na wenzake, na Al-Khiḍr akamuua. Mūsā akamlaumu kwa nguvu na akasema, «vipi umeiua nafsi safi isyokuwa na kosa, isiyofikia umri wa kubeba majukumu, na haijaua mtu mpaka istahili kuuawa? Kwa hakika umefanya jambo baya sana.» info
التفاسير: