Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

Al-Ghashiyah

external-link copy
1 : 88

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡغَٰشِيَةِ

Je, ilikujia,ewe Mtume, habari ya Kiyama chenye vituko venye kuwaenea watu? info
التفاسير:

external-link copy
2 : 88

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ

Nyuso za Makafiri, Siku hiyo, zitakuwa zimenyongeka kwa adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 88

عَامِلَةٞ نَّاصِبَةٞ

Zishughulishie, zimechoka na kutaabika. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 88

تَصۡلَىٰ نَارًا حَامِيَةٗ

Zinachomwa kwa Moto wenye kuwaka kwa ukali. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 88

تُسۡقَىٰ مِنۡ عَيۡنٍ ءَانِيَةٖ

Zitanyweshwa maji ya chemchemi yenye moto sana. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 88

لَّيۡسَ لَهُمۡ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٖ

Watu wa Motoni hawatakuwa na chakula isipokuwa kinachotoka kwenye mti wa miba ilioshikana na chini. Ni kibaya sana chakula hiko na ni kichafu mno. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 88

لَّا يُسۡمِنُ وَلَا يُغۡنِي مِن جُوعٖ

Hakimnoneshi mwenye kukila, awapo amekonda, wala hakimuondolei njaa, awapo na njaa. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 88

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاعِمَةٞ

Nyuso za Waumini, siku ya Kiyama, zitakuwa kwenye neema. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 88

لِّسَعۡيِهَا رَاضِيَةٞ

Kwa kuwa zilijishughulisha ulimwenguni kumtii Mwenyezi Mungu na kuridhika na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 88

فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ

Zitakuwa kwenye Pepo ya daraja ya juu. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 88

لَّا تَسۡمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةٗ

Hutasikia humo hata neno moja la upuuzi. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 88

فِيهَا عَيۡنٞ جَارِيَةٞ

Ndani yake kuna chemchemi yenye kuteremka maji yake. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 88

فِيهَا سُرُرٞ مَّرۡفُوعَةٞ

Ndani yake mna vitanda vilioangatika, info
التفاسير:

external-link copy
14 : 88

وَأَكۡوَابٞ مَّوۡضُوعَةٞ

na vikombe vilivyotayarishwa kwa wenye kunywa, info
التفاسير:

external-link copy
15 : 88

وَنَمَارِقُ مَصۡفُوفَةٞ

na mito iliyopangwa, mmoja baada ya mwingine, info
التفاسير:

external-link copy
16 : 88

وَزَرَابِيُّ مَبۡثُوثَةٌ

na mazulia mengi yaliyotandikwa. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 88

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلۡإِبِلِ كَيۡفَ خُلِقَتۡ

Kwani, hawa makafiri wenye kukanusha, hawaangalii ngamia namna walivyoumbwa kiajabu? info
التفاسير:

external-link copy
18 : 88

وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيۡفَ رُفِعَتۡ

Na mbingu namna zlizoinuliwa juu kwa namna ya kupendeza? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 88

وَإِلَى ٱلۡجِبَالِ كَيۡفَ نُصِبَتۡ

Na milima namna iliyoimarishwa ukapatikana uthabiti na utulivu wa ardhi? info
التفاسير:

external-link copy
20 : 88

وَإِلَى ٱلۡأَرۡضِ كَيۡفَ سُطِحَتۡ

Na ardhi namna ilivyotandikwa na kutayarishwa? info
التفاسير:

external-link copy
21 : 88

فَذَكِّرۡ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٞ

Basi wawaidhie, ewe Mtume, wale wenye kupa nyongo yale uliyotumilizwa kwayo wala usihuzunike kwa kupa mgongo kwao. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 88

لَّسۡتَ عَلَيۡهِم بِمُصَيۡطِرٍ

Kwani wewe ni muwaidhiaji kwao, na si juu yako kuwalazimisha kuamini.. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 88

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ

Lakini yule mwenye kuyapa mgongo makumbusho na mawaidha na akawa mkakamavu kwenye ukafiri wake, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 88

فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلۡعَذَابَ ٱلۡأَكۡبَرَ

Mwenyezi Mungu Atamuadhibu adhabu kali Motoni. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 88

إِنَّ إِلَيۡنَآ إِيَابَهُمۡ

Hakika wao watarudi kwetu baada ya kufa. info
التفاسير:

external-link copy
26 : 88

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا حِسَابَهُم

Kisha ni juu yetu kuwalipa kwa waliyoyafanya. info
التفاسير: