Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

numero y'urupapuro:close

external-link copy
171 : 7

۞ وَإِذۡ نَتَقۡنَا ٱلۡجَبَلَ فَوۡقَهُمۡ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٞ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُۥ وَاقِعُۢ بِهِمۡ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipoliinua jabali juu ya Wana wa Isrāīl likawa kama kwamba ni kiwingu kinachowafinika, wakawa na yakini kuwa kitawaangukia iwapo hawatazikubali hukumu zilizomo kwenye Taurati, na tukawaambia,»Chukueni tulichowapa kwa nguvu.» Yaani, fuateni kivitendo tulichowapa kwa bidii yenu, na yakumbukeni yaliyomo kwenye Kitabu chetu ya ahadi na masharti tuliyoyachukuwa kwenu kwamba mtayatekeleza yaliyomo ndani yake, ili mumche Mola wenu mpate kuokoka na mateso Yake. info
التفاسير:

external-link copy
172 : 7

وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ādam kutoka kwenye migongo ya baba zao, Akawathibitishia upweke Wake kwa kuwatia tabia ya kimaumbile kwamba Yeye ni Mola wao, ni Muumba wao na ni Mmiliki wao; wakamkubalia hilo kwa kuchelea wasije kukanusha Siku ya Kiyama wasikubali chochote katika hilo na wasije wakadai kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu haijasimama kwao na wala hawajui chochote juu yake, bali wao walikuwa wameghafilika na hilo. info
التفاسير:

external-link copy
173 : 7

أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ

Na ili msiseme, «Hakika baba zetu walishirikisha kabla yetu na wakavunja ahadi, na sisi tukawafuata, basi je utatuadhibu kwa yale waliyoyafanya wale ambao waliyaharibu matendo yao kwa kumfanya Mwenyezi Mungu ana mshirika katika ibada?» info
التفاسير:

external-link copy
174 : 7

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na kama tulivyozipambanua hizo aya na tukaeleza ndani yake tulichowafanyia watu waliopita, ndivyo tunavyozipambanua aya na kuzieleza kwa watu wako, ewe Mtume, kwa kutazamia kwamba watarudi waache ushirikina wao na warajee kwa Mola wao. info
التفاسير:

external-link copy
175 : 7

وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱلَّذِيٓ ءَاتَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنۡهَا فَأَتۡبَعَهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ

Na wasimulie,ewe Mtume, watu wako habari ya mwanamume mmoja miongoni mwa Wana wa Isrāīl, tuliyompa hoja zetu na dalili zetu, akajifunza hizo kisha akazikanusha na akazitupa nyuma ya mgongo wake, akashindwa na Shetani na akawa ni miongoni mwa wapotevu wenye kuangamia, kwa sababu ya kuenda kinyume kwake na amri ya Mola wake na kumtii kwake Shetani. info
التفاسير:

external-link copy
176 : 7

وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَيۡهِ يَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ يَلۡهَثۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ

Na lau tulitaka kukitukuza cheo chake kwa aya tulizompa tungalifanya, lakini yeye alitegemea ulimwengu na akafuata matamanio yake, na akafadhilisha ladha zake na hawaa zake juu ya Akhera, na akakataa kumtii Mwenyezi Mungu na akaenda kinyume na amri Yake. Mfano wa mwanamume huyu ni mfano wa mbwa: ukimfukuza au ukimuacha hutoa ulimi wake katika hali zote mbili. Basi hivyo ndivyo alivyo yule aliyejivua aya za Mwenyezi Mungu kwa kuziacha, huwa akiendelea katika ukafiri wake ikiwa utafanya bidii kumlingania au utampuuza. Sifa hii, ewe Mtume, ndiyo sifa ya watu hawa waliokuwa wapotevu kabla hujawajia kwa uongofu na utume. Basi simulia, ewe Mtume, habari za watu waliopita, kwani katika kutolea kwako habari zao ni miujiza mikubwa zaidi; na huenda watu wako wakazingatia juu ya yale uliyowajia nayo na wakakuamini. info
التفاسير:

external-link copy
177 : 7

سَآءَ مَثَلًا ٱلۡقَوۡمُ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَأَنفُسَهُمۡ كَانُواْ يَظۡلِمُونَ

Ni mfano mbaya ulioje! Mfano wa watu waliokanusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake wakazikataa na hali kwamba ni nafsi zao wenyewe walikuwa wakizidhulumu kwa sababu ya kukanusha kwao hoja hizi na dalili. info
التفاسير:

external-link copy
178 : 7

مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِيۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Yule ambaye Mwenyezi Mungu Anamuafikia kumuamini Yeye na kumtii, huyo ndiye aliyeafikiwa; na yule ambaye Anamuachilia Asimuafikiye, huyo ndiye mwenye hasara, mwenye kuangamia. Kuongoza na kupoteza kunatokana na Mwenyezi Mungu Peke Yake. info
التفاسير: