Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

numero y'urupapuro: 443:440 close

external-link copy
55 : 36

إِنَّ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ ٱلۡيَوۡمَ فِي شُغُلٖ فَٰكِهُونَ

Hakika watu wa Peponi Siku hiyo watakuwa wameshughulishwa kwa aina mbalimbali za neema za wao kustarehe nazo, hawawafikirii watu wengine. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 36

هُمۡ وَأَزۡوَٰجُهُمۡ فِي ظِلَٰلٍ عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ

Wao na wake zao watakuwa wanajistarehesha juu ya vitanda vilivyopambwa , na chini ya vivuli vilivyoenea. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 36

لَهُمۡ فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ

Wao Peponi watakuwa na starehe ya matunda yenye ladha ya kila aina, na watakuwa na kila wanalolitaka. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 36

سَلَٰمٞ قَوۡلٗا مِّن رَّبّٖ رَّحِيمٖ

Watakuwa na starehe nyingine kubwa kabisa nayo ni Atakaposema nao Mola wao, Mwenye kuwarehemu kwa kuwasalimia, na hapo watapata amani iliyotimia kwa kila namna. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 36

وَٱمۡتَٰزُواْ ٱلۡيَوۡمَ أَيُّهَا ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Na wataambiwa makafiri Siku hiyo, «Jitengeni na Waumini na mjiepushe nao.» info
التفاسير:

external-link copy
60 : 36

۞ أَلَمۡ أَعۡهَدۡ إِلَيۡكُمۡ يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعۡبُدُواْ ٱلشَّيۡطَٰنَۖ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ

Na Mwenyezi Mungu Atawaambia kwa kuwalaumu na kuwakumbusha, «Kwani sikuwausia, kupitia ndimi za Mitume wetu kwamba msiabudu Shetani wala msimtii? Hakika yeye ni adui ambaye uadui wake umejitokeza wazi. info
التفاسير:

external-link copy
61 : 36

وَأَنِ ٱعۡبُدُونِيۚ هَٰذَا صِرَٰطٞ مُّسۡتَقِيمٞ

«Na nikawaamrisha mniabudu mimi peke yangu, kwani kuniabudu mimi na kunitii na kumuasi Shetani ndiyo Dini iliyonyoka yenye kupelekea kupata radhi zangu na mabustani ya Pepo yangu. info
التفاسير:

external-link copy
62 : 36

وَلَقَدۡ أَضَلَّ مِنكُمۡ جِبِلّٗا كَثِيرًاۖ أَفَلَمۡ تَكُونُواْ تَعۡقِلُونَ

«Hakika Shetani amewapoteza na kuwatoa kwenye haki viumbe wengi kabla yenu. Basi kwani hamkuwa na akili, enyi washirikina, ya kuwakataza nyinyi kumfuata? info
التفاسير:

external-link copy
63 : 36

هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِي كُنتُمۡ تُوعَدُونَ

«Huu ni moto wa Jahanamu ambao mlikuwa mkiahidiwa duniani kwa kumkufuru kwenu Mwenyezi Mungu na kukanusha kwenu Mitume Wake. info
التفاسير:

external-link copy
64 : 36

ٱصۡلَوۡهَا ٱلۡيَوۡمَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡفُرُونَ

«Basi uingieni leo na mteseke kwa joto lake, kwa sababu ya ukafiri wenu! info
التفاسير:

external-link copy
65 : 36

ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٰهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيهِمۡ وَتَشۡهَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Siku hiyo tutaipiga muhuri midomo ya washirikina hawatakuwa ni wenye kusema, na itasema na sisi mikono yao kwa yale iliyoyafanya ya maonevu, na itatoa ushahidi miguu yao kwa yale iliyoyaendea duniani na dhambi ilizozichuma. info
التفاسير:

external-link copy
66 : 36

وَلَوۡ نَشَآءُ لَطَمَسۡنَا عَلَىٰٓ أَعۡيُنِهِمۡ فَٱسۡتَبَقُواْ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبۡصِرُونَ

Na lau tutataka tutayafuta macho yao na kuondoa maangalizi yao, kama tulivyoifunga midomo yao, hapo waikimbilie njia ya Ṣirāṭ ili waivuke. Basi vipi hilo litakuwa kwao na hali macho yao yamefutwa hayaoni? info
التفاسير:

external-link copy
67 : 36

وَلَوۡ نَشَآءُ لَمَسَخۡنَٰهُمۡ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمۡ فَمَا ٱسۡتَطَٰعُواْ مُضِيّٗا وَلَا يَرۡجِعُونَ

Na lau tunataka tutaligeuza umbo lao na kuwakalisha mahali pao, wasiweze kuenda mbele wala kurudi nyuma. info
التفاسير:

external-link copy
68 : 36

وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَكِّسۡهُ فِي ٱلۡخَلۡقِۚ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ

Na yoyote tutakayeurefusha umri wake mpaka awe mkongwe tunamrudisha kwenye hali ya udhaifu wa akili na udhaifu wa mwili. Basi hawatii akilini kwamba yule Aliyefanya hili ni mwenye uweza wa kuwafufua? info
التفاسير:

external-link copy
69 : 36

وَمَا عَلَّمۡنَٰهُ ٱلشِّعۡرَ وَمَا يَنۢبَغِي لَهُۥٓۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ وَقُرۡءَانٞ مُّبِينٞ

Na hatukumfundisha mjumbe wetu Muhammad mashairi, na haipasi kwake kuwa mshairi. Haikuwa hii aliokuja nayo isipokuwa ni Ukumbusho kwa wale wenye busara kujikumbusha nao na ni Qur’ani yenye kufafanua haki na batili, hukumu zake ziko wazi, na pia hekima zake na mawaidha yake, info
التفاسير:

external-link copy
70 : 36

لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيّٗا وَيَحِقَّ ٱلۡقَوۡلُ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

ili imuonye ambaye moyo wake uko hai na akili yake ina nuru, na ili ithibiti adhabu kwa wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, kwa kuwa wao, kwa hii Qur’ani, hoja ya Mwenyezi Mungu ya mkato imewasimamia. info
التفاسير: