Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

Luqman

external-link copy
1 : 31

الٓمٓ

«Alif, Lām, Mīm» Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqrah. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 31

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡحَكِيمِ

Aya hizi ni aya za Qur’ani yenye hekima kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 31

هُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّلۡمُحۡسِنِينَ

Aya hizi ni uongofu na ni rehema kwa waliofanya vizuri kuyafiuata kivitendo yale yaliyoteremshwa katika Qur’ani na aliyowaamrisha kwayo Mtume wao Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 31

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ

Wanaotekeleza Swala kikamilifu kwa nyakati zake na wanaotoa Zaka zilizo lazima juu yao kwa wanaostahiki kupewa. Na hali wao wana yakini kuwa kuna kufufuliwa na kulipwa Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 31

أُوْلَٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Hao wanaosifika kwa sifa zilizotangulia wako kwenye ubainifu na nuru kutoka kwa Mola wao, na wao ndio wenye kufaulu ulimwenguni na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 31

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَشۡتَرِي لَهۡوَ ٱلۡحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na miongoni mwa watu kuna anayenunua maneno ya pumbao, nayo ni kila chenye kumpumbaza mtu na utiifu wa Mwenyezi Mungu, ili awapoteze watu na njia ya uongofu wafuate njia ya matamanio na azifanye aya za Mwenyezi Mungu kuwa ni shere, basi hao watakuwa na adhabu yenye kuwadhalilisha na kuwatweza. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 31

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا وَلَّىٰ مُسۡتَكۡبِرٗا كَأَن لَّمۡ يَسۡمَعۡهَا كَأَنَّ فِيٓ أُذُنَيۡهِ وَقۡرٗاۖ فَبَشِّرۡهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Na anaposomewa aya za Qur’ani anaupa mgongo utiifu wa Mwenyezi Mungu na anafanya kiburi bila kuzingatia, kama kwamba yeye hakusikia kitu, kama kwamba kwenye mashikio yake kuna uziwi. Na yoyote ambaye hali yake ni hii, mpe bishara, ewe Mtume, ya adhabu kali yenye kuumiza humo Motoni Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 31

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتُ ٱلنَّعِيمِ

Hakika wale waliomuamini mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wakatenda mema waliyoamrishwa, hao wana starehe ya daima ndani ya mabustani ya Peponi. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 31

خَٰلِدِينَ فِيهَاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na uhai wao katika mabustani hayo ya Peponi ni uhai wa milele, haukatiki wala haumaliziki, Mwenyezi Mungu Amewaahidi hilo ahadi ya kweli. Na Yeye , kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Haendi kinyume na ahadi Yake. Na Yeye ni Mshindi katika amri Yake, ni Mwenye hekima katika uendeshaji mambo Wake. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 31

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيۡرِ عَمَدٖ تَرَوۡنَهَاۖ وَأَلۡقَىٰ فِي ٱلۡأَرۡضِ رَوَٰسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمۡ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَآبَّةٖۚ وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجٖ كَرِيمٍ

Ameumba mbingu, Akaziinua bila ya nguzo kama mnavyoziona. Na Ameweka ndani ya ardhi majabali yaliyojikita, ili zisipate kutikisika na kutetemeka yakaharibika maisha yenu. Na Ameeneza kwenye ardhi aina mbalimbali za wanyama. Na tumeteremsha kutoka mawinguni mvua, tukaotesha kwayo kwenye ardhi kila aina ya mimea mizuri yenye nafuu yenye mandhari mazuri. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 31

هَٰذَا خَلۡقُ ٱللَّهِ فَأَرُونِي مَاذَا خَلَقَ ٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦۚ بَلِ ٱلظَّٰلِمُونَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Na vyote mnavyovishuhudia ni viumbe vya Mwenyezi Mungu, basi nionesheni, enyi washirikina, imeumba nini hiyo miungu yenu mnayoiabudu badala ya Mwenyezi Mungu? Bali washirikina wameenda kando na haki na msimamo wa sawa waziwazi. info
التفاسير: