Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis

external-link copy
39 : 30

وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن رِّبٗا لِّيَرۡبُوَاْ فِيٓ أَمۡوَٰلِ ٱلنَّاسِ فَلَا يَرۡبُواْ عِندَ ٱللَّهِۖ وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن زَكَوٰةٖ تُرِيدُونَ وَجۡهَ ٱللَّهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُضۡعِفُونَ

Na mkopo wowote wa pesa mnaoutoa kwa makusudio ya riba, na kutaka kuzidisha mkopo huo ili kupatikane ongezeko katika mali ya watu, basi mbele ya Mwenyezi Mungu hayaongezeki, bali Anayaondolea baraka na kuyabatilisha. Na Zaka na sadaka mnazotoa kuwapatia wastahiki kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na kutaka malipo yake, basi hiki ndicho ambacho Mwenyezi Mungu Anakikubali na Atawaongezea mara nyingi zaidi. info
التفاسير: