Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução em Swahili - Áli Muhsin

external-link copy
147 : 3

وَمَا كَانَ قَوۡلَهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسۡرَافَنَا فِيٓ أَمۡرِنَا وَثَبِّتۡ أَقۡدَامَنَا وَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Wala kauli yao haikuwa ila ni kusema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. info

Na kauli yao vilipo kuwa vita vikali haikuwa ila kusema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe dhambi zetu kubwa na ndogo. Na tusimamishe imara katika midani za vita, na utunusuru na hawa maadui wa Dini yako, wenye kukukanya Wewe na ujumbe wa Mtume wako.

التفاسير: