Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução em Swahili - Áli Muhsin

external-link copy
241 : 2

وَلِلۡمُطَلَّقَٰتِ مَتَٰعُۢ بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُتَّقِينَ

Na wanawake walio achwa wapewe cha kuwaliwaza kwa mujibu wa Sharia. Haya ni waajibu kwa wachamngu. [241] info

[241] Na wanawake walio pewa T'alaka baada ya kuingia harusi wana haki wapewe mali ya kuwaliwaza. Wapewe kwa wema, kwa kadiri ya utajiri na umasikini wa mume. Kumcha Mwenyezi Mungu kunawajibisha hayo, na pia watu wa Imani wanalazimika na hayo.

التفاسير: