Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
11 : 21

وَكَمۡ قَصَمۡنَا مِن قَرۡيَةٖ كَانَتۡ ظَالِمَةٗ وَأَنشَأۡنَا بَعۡدَهَا قَوۡمًا ءَاخَرِينَ

Na kuna miji mingi ambayo watu wake walikuwa madhalimu kwa kukanusha kwao yale ambayo Mitume wao walikuja nayo. Ndipo tukawaangamiza kwa adhabu iliyowamaliza wote, na tukafanya wapatikane watu wengine wasiokuwa wao. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 21

فَلَمَّآ أَحَسُّواْ بَأۡسَنَآ إِذَا هُم مِّنۡهَا يَرۡكُضُونَ

Walipoiyona, madhalimu hawa, adhabu yetu kali ikiwashukia na wakaziona ishara zake, wakitahamaki wakawa wanakimbia kwa haraka kutoka mjini mwao. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 21

لَا تَرۡكُضُواْ وَٱرۡجِعُوٓاْ إِلَىٰ مَآ أُتۡرِفۡتُمۡ فِيهِ وَمَسَٰكِنِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تُسۡـَٔلُونَ

Wakaitwa wakiwa katika hali hii na kuambiwa, «Msikimbieni, na rudini kwenye ladha zenu na starehe zenu katika ulimwengu wenu wenye kupumbaza na nyumba zenu zilizojengwa, kwani huenda mkaulizwa jambo kuhusu ulimwengu wenu. Na hiyo ni kwa njia ya kuwafanyia shere na ubishi.» info
التفاسير:

external-link copy
14 : 21

قَالُواْ يَٰوَيۡلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Hawakuwa na majibu yoyote isipokuwa ni kukubali makosa yao na kusema, «Ee maangamivu yetu! Tumejidhulumu nafsi zetu kwa ukafiri wetu.» info
التفاسير:

external-link copy
15 : 21

فَمَا زَالَت تِّلۡكَ دَعۡوَىٰهُمۡ حَتَّىٰ جَعَلۡنَٰهُمۡ حَصِيدًا خَٰمِدِينَ

Yaliendelea maneno hayo - nayo ni yale ya kujiapiza wenyewe maangamivu na kukubali kuwa wamejidhulumu wenyewe- kuwa ndiyo mwito wao wanaoukariri mpaka tukawafanya kama mimea ya ukulima iliyovunwa, wakiwa wametulia hawana uhai. Basi kuweni na hadhari, enyi mnaoambiwa, na kuendelea kumkanusha Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, isije ikawashukia nyinyi yale yaliyowashukia watu waliopita kabla yenu. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 21

وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا لَٰعِبِينَ

Na hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyoko baina yake kwa upuuzi na ubatilifu, lakini ni kwa kusimamisha hoja juu yenu, enyi watu, na ili mzingatie kwa hayo yote mpate kujua kwamba Yule Aliyeziumba hizo mbingu na ardhi hafanani na chochote, na hakuna anayefaa kuabudiwa isipokuwa Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 21

لَوۡ أَرَدۡنَآ أَن نَّتَّخِذَ لَهۡوٗا لَّٱتَّخَذۡنَٰهُ مِن لَّدُنَّآ إِن كُنَّا فَٰعِلِينَ

Lau tulitaka kujifanyia kipumbazi cha mtoto au mke tungalikifanya kutoka kwetu, na sio kwenu. Hatukuwa ni wenye kufanya hilo kwa kuwa ni muhali kwetu kuwa na mtoto au mke. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 21

بَلۡ نَقۡذِفُ بِٱلۡحَقِّ عَلَى ٱلۡبَٰطِلِ فَيَدۡمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٞۚ وَلَكُمُ ٱلۡوَيۡلُ مِمَّا تَصِفُونَ

bali tunaisukuma haki na tunaifafanua, na hapo urongo unapomoka, na punde si punde unaondoka na kupotea. Na nyinyi, enyi washirikina, mtapata adhabu huko Akhera kwa kumsifu kwenu Mola wenu kwa sifa zisizonasibiana na Yeye. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 21

وَلَهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَمَنۡ عِندَهُۥ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسۡتَحۡسِرُونَ

Ni milki ya Mweyezi Mungu, Aliyetakasika na sifa za upungufu, kila aliye mbinguni na ardhini. Na wale Malaika walioko mbele Yake hawafanyi kiburi kumuabudu Yeye wala hawachoki kufanya hivyo. Basi vipi itafaa Ashirikishwe na kitu ambacho ni mja wake na kiumbe chake. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 21

يُسَبِّحُونَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ لَا يَفۡتُرُونَ

Wao (hao Malaika) wanamtaja Mwenyezi Mungu na wanamtakasa daima, hawadhoofiki wala hawachoki. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 21

أَمِ ٱتَّخَذُوٓاْ ءَالِهَةٗ مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ هُمۡ يُنشِرُونَ

Itakuwa sawa vipi kwa washirikina kujifanyia waungu walemevu kutoka ardhini wasioweza kuhuisha wafu? info
التفاسير:

external-link copy
22 : 21

لَوۡ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَاۚ فَسُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلۡعَرۡشِ عَمَّا يَصِفُونَ

Lau mbinguni na ardhini kulikuwa na waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, wenye kuyaendesha mambo yake, ungaliharibika mpango wake. Basi Mwenyezi Mungu, Bwana wa 'Arsh, Ameepukakana na sifa za upungufu na Ametakasika na kila sifa ambayo wakanushaji makafiri wanamsifu nayo ya urongo, uzushi na kila aibu. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 21

لَا يُسۡـَٔلُ عَمَّا يَفۡعَلُ وَهُمۡ يُسۡـَٔلُونَ

Miongoni mwa dalili za kupwekeka Kwake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kuumba na kustahiki kuabudiwa ni kwamba Yeye Haulizwi kuhusu uamuzi Wake kwa viumbe Wake na kwamba viumbe Wake wote ndio wenye kuulizwa kuhusu matendo yao. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 21

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةٗۖ قُلۡ هَاتُواْ بُرۡهَٰنَكُمۡۖ هَٰذَا ذِكۡرُ مَن مَّعِيَ وَذِكۡرُ مَن قَبۡلِيۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ٱلۡحَقَّۖ فَهُم مُّعۡرِضُونَ

Je, hawa washirikina waliwafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu wanaonufaisha na kudhuru na wanaohuisha na kufisha? Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Leteni dalili zenu mlizonazo juu ya hao mliowafanya waungu.» Kwani hakuna, ndani ya Qur’ani niliyokuja nayo wala ndani ya Vitabu vilivyotangulia, dalili yoyote ya yale mliyoyafuata.» Na wao hawakushirikisha isipokuwa ni kwa sababu ya ujinga wao na kuigiza, kwa hivyo wao ni wenye kuupa mgongo ukweli na ni wenye kuukataa. info
التفاسير: