Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

external-link copy
50 : 17

۞ قُلۡ كُونُواْ حِجَارَةً أَوۡ حَدِيدًا

Waambie, ewe Mtume, kwa njia ya kuwafanya washindwe, «Kuweni na nguvu na ugumu kama mawe au chuma mkiweza hilo. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 17

أَوۡ خَلۡقٗا مِّمَّا يَكۡبُرُ فِي صُدُورِكُمۡۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَاۖ قُلِ ٱلَّذِي فَطَرَكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖۚ فَسَيُنۡغِضُونَ إِلَيۡكَ رُءُوسَهُمۡ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَۖ قُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبٗا

Au kuweni umbo lolote kubwa ambalo akili zenu zaliona kuwa liko mbali na uhakika.» Na watasema kwa kukanusha, «Ni nani atakayeturudisha kwenye uhai baada ya kufa?» Waambie, «Atakayewarudisha na kuwarejesha ni Mwenyezi Mungu Aliyewaumba kutoka kwenye hali ya kutokuwako mara ya kwanza.» Na wasikiapo majibu haya watatikisa vichwa vyao kwa njia ya shere, huku wakiona ajabu na watasema, wakiliona jambo hilo kuwa ni mbali kukubalika, «Ufufuzi huu utatukia lini?» Sema, «Ni lipi linalowajulisha kwamba Ufufuzi huu, mnaoukanusha na mnaouona kuwa uko mbali, huenda ukawa ni wenye kutukia kipindi cha karibu?» info
التفاسير:

external-link copy
52 : 17

يَوۡمَ يَدۡعُوكُمۡ فَتَسۡتَجِيبُونَ بِحَمۡدِهِۦ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا

Siku Atakapowaita Muumba wenu mtoke kwenye makaburi yenu na mkaitika amri ya Mwenyezi Munguna na mkaiyandama, na shukrani ni Zake kwa kila namna, na mkadhani, kwa kituko cha Siku ya Kiyama na kwa kipindi kirefu cha kukaa kwenu Akhera, kwamba nyinyi hamkukaa duniani isipokuwa muda mchache. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 17

وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُواْ ٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ يَنزَغُ بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ كَانَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٗا مُّبِينٗا

Na waambie waja wangu Waumini waseme, katika mazungumzo yao na kushauriana kwao wao kwa wao, maneno mazuri, kwani wao wakitofanya hivyo Shetani atatia ugomvi, uharibifu na utesi baina yao. Hakika Shetani kwa binadamu ni adui aliyeudhihirisha uadui. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 17

رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِكُمۡۖ إِن يَشَأۡ يَرۡحَمۡكُمۡ أَوۡ إِن يَشَأۡ يُعَذِّبۡكُمۡۚ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا

Mola wenu Anawajua nyinyi zaidi, enyi watu, Akitaka Atawarehemu Awaafikie kwenye Imani au Akitaka atawafisha kwenye ukafiri kisha Awaadhibu. Na hatukukutumiliza, ewe Mtume, uwe ni muwakilishi juu yao, unayapanga mambo yao na unawalipa kwa matendo yao, jukumu lako ni kuyafikisha uliyotumilizwa kwayo na kuieleza njia iliyolingana sawa. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 17

وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِمَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ فَضَّلۡنَا بَعۡضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعۡضٖۖ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا

Na Mola wako, ewe Mtume, Anawajua zaidi walioko mbinguni na ardhini, na tumewafadhilisha baadhi ya Mitume juu ya wengine kwa matukufu, wingi wa wafuasi na kuwateremshia Vitabu, na Dawud, amani imshukiye, tumempa Zaburi. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 17

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمۡلِكُونَ كَشۡفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمۡ وَلَا تَحۡوِيلًا

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina wa Makkah, «Hawa masanamu mnaowaita wawaondolee shida hawawezi hilo wala hawawezi kuiyepusha kwenu nyinyi kuipeleka kwa wengine, na pia hawawezi kuigeuza kutoka namna ilivyo kuifanya namna nyingine, Mwenye kuweza hilo ni Mwenyezi Mungu Peke Yake.» Aya hii inakusanya kila anayeombwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa Manabii, watu wema na wasiokuwa hao, kwa tamko la istighāthah (kutaka uokozi) au du'a’ (maombi) au mfano wake, kwani hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 17

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ يَبۡتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلۡوَسِيلَةَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ وَيَرۡجُونَ رَحۡمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحۡذُورٗا

Hao ambao washirikina wanawaomba, miongoni mwa Manabii, watu wema na Malaika, wao wenyewe wanashindana kujiweka karibu na Mola wao kwa matendo mema wanayoyaweza, wanatarajia rehema Yake na wanaogopa adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako ndiyo ambayo inatakikana kwa waja wawe na hadhari nayo na waiogope. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 17

وَإِن مِّن قَرۡيَةٍ إِلَّا نَحۡنُ مُهۡلِكُوهَا قَبۡلَ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَوۡ مُعَذِّبُوهَا عَذَابٗا شَدِيدٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا

Na Mwenyezi Mungu Anawaonya wanaokufuru kwamba hakuna mji wowote wenye kukufuru na kukanusha Mitume isipokuwa mateso Yake yataushukia kwa maangamivu hapa duniani kabla ya Siku ya Kiyama au kwa adhabu kali juu ya watu wake. Hayo ni maandishi Aliyoyaandika Mwenyezi Mungu na hukumu Aliyoipitisha, hapana budi kujiri, nayo imeandikwa kwenye Al-Lawḥ Al-Mahfūḍ (Ubao Uliohifadhiwa). info
التفاسير: