د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

د مخ نمبر:close

external-link copy
164 : 7

وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ

Na kikundi miongoni mwao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola wenu Mlezi, na huenda nao wakamcha Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
165 : 7

فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦٓ أَنجَيۡنَا ٱلَّذِينَ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلسُّوٓءِ وَأَخَذۡنَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ بِعَذَابِۭ بَـِٔيسِۭ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ

Basi walipoyasahau yale waliyokumbushwa kwayo, tukawaokoa wale waliokuwa wakikataza mabaya, na tukawachukua wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya mno kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka. info
التفاسير:

external-link copy
166 : 7

فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُهُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ

Walipotakabari na kuasi yale waliyokatazwa, tukawaambia, "Kuweni manyani, mliodharauliwa." info
التفاسير:

external-link copy
167 : 7

وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبۡعَثَنَّ عَلَيۡهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَن يَسُومُهُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na pale alipotangaza Mola wako Mlezi kwamba hakuna shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
168 : 7

وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ

Na tukawagawanya katika ardhi umma mbalimbali. Miongoni mwao kuna wale walio wema, na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mazuri na mabaya huenda wakarejea. info
التفاسير:

external-link copy
169 : 7

فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٞ وَرِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَأۡخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلۡأَدۡنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغۡفَرُ لَنَا وَإِن يَأۡتِهِمۡ عَرَضٞ مِّثۡلُهُۥ يَأۡخُذُوهُۚ أَلَمۡ يُؤۡخَذۡ عَلَيۡهِم مِّيثَٰقُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِۗ وَٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ

Basi wakafuatia baada yao wafuatizi waliokirithi Kitabu. Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema, "Tutasitiriwa dhambi!" Na ikiwajia tena anasa mfano wake, wanaichukua pia. Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu? Nao wamekwishasoma yale yaliyo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao. Basi je, hamtii akilini? info
التفاسير:

external-link copy
170 : 7

وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Na wale wanaokikamata sawasawa Kitabu, na wakasimamisha Swala, hakika Sisi hatupotezi ujira wa watengenezao. info
التفاسير: