د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمة مرکز

د مخ نمبر:close

external-link copy
138 : 7

وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتَوۡاْ عَلَىٰ قَوۡمٖ يَعۡكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصۡنَامٖ لَّهُمۡۚ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱجۡعَل لَّنَآ إِلَٰهٗا كَمَا لَهُمۡ ءَالِهَةٞۚ قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ

Na tukawavusha bahari Wana wa Israili, kisha wakajia kaumu waliokuwa wanayaabudu masanamu yao. Wakasema, "Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Musa akasema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu. info
التفاسير:

external-link copy
139 : 7

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٞ مَّا هُمۡ فِيهِ وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hakika hawa, haya waliyomo yatakujaangamia, na ni batili hayo waliyokuwa wakiyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
140 : 7

قَالَ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِيكُمۡ إِلَٰهٗا وَهُوَ فَضَّلَكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ

Akasema, "Je, niwatafutie mungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye aliyewaboresha kuliko walimwengu wote?" info
التفاسير:

external-link copy
141 : 7

وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ

Na pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya zaidi. Wakiwaua wavulana wenu, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi. info
التفاسير:

external-link copy
142 : 7

۞ وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Na tulimuahidi Musa usiku thelathini na tukazitimiza kwa kumi; basi ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi usiku arobaini. Na Musa akamwambia kaka yake, Haarun: Shika pahali pangu katika kaumu yangu na utengeneze, wala usifuate njia ya waharibifu. info
التفاسير:

external-link copy
143 : 7

وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَٰتِنَا وَكَلَّمَهُۥ رَبُّهُۥ قَالَ رَبِّ أَرِنِيٓ أَنظُرۡ إِلَيۡكَۚ قَالَ لَن تَرَىٰنِي وَلَٰكِنِ ٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡجَبَلِ فَإِنِ ٱسۡتَقَرَّ مَكَانَهُۥ فَسَوۡفَ تَرَىٰنِيۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُۥ لِلۡجَبَلِ جَعَلَهُۥ دَكّٗا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقٗاۚ فَلَمَّآ أَفَاقَ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ تُبۡتُ إِلَيۡكَ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na alipokuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamuongelesha, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutaniona. Lakini utazame huo mlima. Ikiwa utabaki mahali pake, basi utaniona. Basi alipojionyesha Mola wake Mlezi kwa mlima huo, akaufanya upasukepasuke, na Musa akaanguka chini akazimia. Basi alipozindukana, akasema: Subhanaka (Umetakasika)! Nimetubia kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini. info
التفاسير: