د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

د مخ نمبر:close

external-link copy
90 : 23

بَلۡ أَتَيۡنَٰهُم بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Ilivyo ni kwamba tumewaletea wakanushaji hawa ukweli wa yale tuliyompeleka kwayo Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Na kwa hakika wao ni warongo kwenye ushirikina wao na ukanushaji wao kufufuliwa. info
التفاسير:

external-link copy
91 : 23

مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدٖ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنۡ إِلَٰهٍۚ إِذٗا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَٰهِۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعۡضُهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Mwenyezi Mungu Hakujifanyia mwana, na hakukuwa pamoja na Yeye muabudiwa mwingine, kwani kama kungalikuwa huko kuna waabudiwa zaidi ya mmoja pamoja na Yeye, basi kila muabudiwa angalijitenga na alivyoviumba na kungalikuwa na ushindani kati yao kama ilivyo kwa watawala wa ulimwnguni. Hapo mpango wa ulimwengu ungaliharibika. Ametakasika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kuepukana na sifa wanazompa za kuwa Yeye ana mshirika au mwana. info
التفاسير:

external-link copy
92 : 23

عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Yeye, Peke Yake, Ndiye Anayejua yanayofichika kwa viumbe vyake na wanayoyaona. Basi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameepukana na mshirika ambaye wanadai kuwa Anaye. info
التفاسير:

external-link copy
93 : 23

قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ

Sema, ewe Mtume, «Mola wangu! Unioneshapo kwa hawa washirikina ile adhabu yako uliyowaonya nayo, info
التفاسير:

external-link copy
94 : 23

رَبِّ فَلَا تَجۡعَلۡنِي فِي ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

basi usiniangamize kwa ile uliyowaangamiza nayo. Na uniokoe na adhabu yako na hasira zako. Usiniweke pamoja na watu washirikina na madhalimu. Bali niingize kwa wale uliokuwa radhi nao.» info
التفاسير:

external-link copy
95 : 23

وَإِنَّا عَلَىٰٓ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمۡ لَقَٰدِرُونَ

Na kwa hakika sisi tunaweza kukuonesha yale tunayowaahidi ya adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 23

ٱدۡفَعۡ بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُ ٱلسَّيِّئَةَۚ نَحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَصِفُونَ

Pindi wanapokufanyia ubaya maadui zako, ewe Mtume, kwa maneno au vitendo, basi usiwalipe ubaya, lakini uondoshe ubaya wao kwa kuwafanyia wema. Sisi tunayajua mno yale wanayokubandika washirikina ya sifa za ushirikina na kukukanusha, na Atawalipa kwa hayo malipo maovu mno. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 23

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنۡ هَمَزَٰتِ ٱلشَّيَٰطِينِ

Na useme, ewe Nabii, «Mola wangu! Najilinda kwako na upotezaji wa Mashetani unaoupelekea kwenye ubatilifu na uharibifu na kuzuia watu wasiifuate haki. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 23

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحۡضُرُونِ

Na ninajilinda kwako, ewe Mola wangu, na kuingiliwa na wao kwenye mambo yangu.» info
التفاسير:

external-link copy
99 : 23

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ رَبِّ ٱرۡجِعُونِ

Mwenyezi Mungu Anawatolea habari makafiri au waliokiuka mipaka ya amri Yake, Aliyetukuka, walioko kwenye hali ya kusongwa na kifo, mauti yalipowafikia na wakaishuhudia adhabu waliyoandaliwa, hapo huwa akisema kila mmoja wao, «Mola wangu! Nirudisha ulimwenguni. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 23

لَعَلِّيٓ أَعۡمَلُ صَٰلِحٗا فِيمَا تَرَكۡتُۚ كَلَّآۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَآئِلُهَاۖ وَمِن وَرَآئِهِم بَرۡزَخٌ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ

«Huenda mimi nikayarekebisha yale niliyoyapoteza ya imani na utiifu.» Hatolipata hilo, kwani hatakubaliwa hilo aliloliomba wala hatapewa muhula. Hilo ni neno tu atalisema. Ni neno lisilomnufaisha, na yeye kwa neno hilo si mkweli, kwani lau angalirudishwa ulimwenguni angaliyarudia yale aliyokatazwa. Na Wenye kufa watasalia kwenye kizuizi na kitengo kilichoko kati ya Akhera na duniani mpaka Siku ya kufufuliwa na kukusanywa. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 23

فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ فَلَآ أَنسَابَ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ وَلَا يَتَسَآءَلُونَ

Basi Siku ya Kiyama itakapokuwa, na Malaika anayehusika akavivia kwenye baragumu, na watu wakafufuliwa kutoka makaburini mwao, hapo hakuna kujigamba kwa nasaba kama walivyokuwa wakijigamba nazo duniani wala hapana yoyote atakayemuuliza yoyote. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 23

فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Basi yule ambaye mema yake yatakuwa mengi na zikawa nzito kwayo mizani za matendo yake Siku ya kuhesabiwa, basi hao ndio wenye kufaulu kupata Pepo. info
التفاسير:

external-link copy
103 : 23

وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فِي جَهَنَّمَ خَٰلِدُونَ

Na yule ambaye mema yake yatakuwa machache kwenye mizani na maovu yake yatakuwa mengi zaidi, na kubwa zaidi ya hayo maovu ni ushirikina, basi hao ndio ambao wamepita patupu na wakaziangamiza nafsi zao kwenye moto wa Jahanamu, watasalia humo milele. info
التفاسير:

external-link copy
104 : 23

تَلۡفَحُ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ وَهُمۡ فِيهَا كَٰلِحُونَ

Moto huo utaunguza nyuso zao, na wao humo watakuwa ni wenye kufinya nyuso, midomo yao imekauka na meno yao yamejitokeza nje. info
التفاسير: