ߞߎ߬ߙߣߊ߬ ߞߟߊߒߞߋ ߞߘߐ ߟߎ߬ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߛߥߊߤߟߌ ߘߟߊߡߌߘߊ - ߊ߳ߺߊ߬ߟߌ߯ ߡߎߤ߭ߑߛߌߣߎ߫ ߊ.ߟߑߓߊߙߎ߯ߣߌ߮ ߓߟߏ߫

ߞߐߜߍ ߝߙߍߕߍ:close

external-link copy
87 : 9

رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ

Wameridhia kuwa pamoja na wabakiao nyuma, na nyoyo zao zikapigwa muhuri; kwa hivyo hawafahamu. info

Hao hakika wamejikubalia wenyewe wahisabike katika walio bakia nyuma, nao ni wanawake, na wasio jiweza, na watoto wadogo wasio viweza vita. Na Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao kwa khofu na unaafiki. Basi hao hawafahamu vilivyo uhakika wa Jihadi na kumfuata Mtume, nako ni kupata utukufu duniani na kupata radhi ya Mwenyezi Mungu katika Akhera.

التفاسير:

external-link copy
88 : 9

لَٰكِنِ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ جَٰهَدُواْ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡخَيۡرَٰتُۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Lakini Mtume na wale walio amini pamoja naye waliwania Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio watakao pata kheri nyingi, na hao ndio wenye kufanikiwa. info

Hiyo ndiyo hali ya wanaafiki. Lakini Mtume na wale walio sadiki pamoja naye, wametoa mali zao na roho zao ili kumridhi Mwenyezi Mungu, na kulinyanyua Neno lake. Hao tu peke yao ndio watakao pata kila kheri ya duniani, nayo ni utukufu na ushindi, na a'mali njema. Na wao peke yao ndio wenye kufuzu.

التفاسير:

external-link copy
89 : 9

أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Mwenyezi Mungu amewatengenezea Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa. info

Na Mwenyezi Mungu amekwisha watengenezea katika Akhera neema za kudumu, katika Mabustani yanayo pitiwa na mito. Na huko ndiko kufuzu adhimu, na kufanikiwa kukubwa.

التفاسير:

external-link copy
90 : 9

وَجَآءَ ٱلۡمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ لِيُؤۡذَنَ لَهُمۡ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۚ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Na walikuja wenye kutoa udhuru katika Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale walio mwambia Mwenyezi Mungu na Mtume wake uwongo. Itawafika walio kufuru katika wao adhabu chungu. info

Na kama walivyo bakia nyuma baadhi ya wanaafiki katika Madina wasitoke kwenda pigana Jihadi, kadhaalika walikuja baadhi ya Mabedui, nao ni watu wa majangwani, wakijidai kutoa udhuru huu na huu ili waruhusiwe wabaki nyuma. Na kwa hivyo wakakaa nyuma wale walio mwambia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuonyesha Imani. Hawakuhudhuria, wala hawakumtaka udhuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ni dalili ya ukafiri wao. Adhabu ya kutia uchungu itawateremkia walio makafiri kati yao.

التفاسير:

external-link copy
91 : 9

لَّيۡسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلۡمَرۡضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُواْ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ مِن سَبِيلٖۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Hapana lawama kwa wanyonge, wagonjwa, na wasio pata cha kutumia, maadamu wanamsafia niya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana njia ya kuwalaumu wanao fanya wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. info

Hakika wanao kubaliwa udhuru wao kubaki nyuma ni wanyonge, na madhaifu wasio jiweza, na wagonjwa, na mafakiri wasio pata cha kutumia kujizatiti kwa vita. Na watu hawa wakiwa wao wana usafi wa niya kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika Dini yao, basi hao ni watu wema, wala hapana lawama juu ya watu wema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Maghfira, na Mkunjufu wa Rehema.

التفاسير:

external-link copy
92 : 9

وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوۡكَ لِتَحۡمِلَهُمۡ قُلۡتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحۡمِلُكُمۡ عَلَيۡهِ تَوَلَّواْ وَّأَعۡيُنُهُمۡ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمۡعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُواْ مَا يُنفِقُونَ

Wala wale walio kujia ili uwachukue ukasema: Sina kipando cha kukuchukueni. Tena wakarudi na macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kukosa cha kutoa. info

Na kadhaalika hapana lawama juu ya Waumini wanao kujia uwapatie kipando cha kwendea Jihadi ukawaambia: Sina cha kukupandisheni. Wakenda zao na macho yao yanatiririka machozi kwa huzuni ya kukosa sharafu ya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa kukosa kwao masurufu ya kutoa.

التفاسير:

external-link copy
93 : 9

۞ إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسۡتَـٔۡذِنُونَكَ وَهُمۡ أَغۡنِيَآءُۚ رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Ipo njia ya kuwalaumu wale wanao kuomba ruhusa wasende vitani na hali wao ni matajiri. Wameridhia kuwa pamoja na wanao bakia nyuma. Na Mwenyezi Mungu amewapiga muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawajui. info

Lawama na adhabu ni juu ya wale wanao kutaka ruhusa, ewe Mtume, wabakie nyuma wasende vitani, nao wanayo mali na zana, na wanaweza kutoka pamoja nawe. Kwani hao juu ya uwezo wao wamekhiari wabaki nyuma pamoja na wanawake wanyonge, na wazee wakongwe, na wagonjwa wasio jiweza; na nyoyo zao hao zimefungwa hazitambui Haki, na hawajui matokeo maovu kabisa yatakayotokea duniani na Akhera kwa kule kuacha kutoka kwao kwenda kwenye Jihadi.

التفاسير: