पवित्र कुरअानको अर्थको अनुवाद - स्वाहिली अनुवाद : अली मुहसिन बरवानी ।

Al-Isra

external-link copy
1 : 17

سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِيٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلٗا مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِي بَٰرَكۡنَا حَوۡلَهُۥ لِنُرِيَهُۥ مِنۡ ءَايَٰتِنَآۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona. info

Mwenyezi Mungu aliye takasika na kila ambalo lisio laiki naye. Yeye ndiye aliye mchukua mja wake Muhammad wakati wa usiku kutoka Msikiti Mtakatifu wa Makka kwendea Msikiti wa Mbali wa Baitul Muqaddas, ambao tuliwabarikia wakaazi majirani wa Msikiti huo katika mahitaji yao, ili tumwonyeshe baadhi ya Ishara zetu zenye ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa Mimi ni Mungu Mmoja peke yangu, na ukubwa wa uwezo wangu! Hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

التفاسير:

external-link copy
2 : 17

وَءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ وَجَعَلۡنَٰهُ هُدٗى لِّبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ أَلَّا تَتَّخِذُواْ مِن دُونِي وَكِيلٗا

Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi! info

Na hakika hiyo Baitul Muqaddas ilikuwa inakaliwa na Wana wa Israili baada ya Musa, mpaka walipo fanya fisadi yao humo, wakafukuzwa hapo zamani. Haya ijapo kuwa Sisi tulimpa Musa Taurati, na tukatia ndani yake uwongofu, na tukawaambia: Msimfanye yeyote wa kumtegemezea mambo yenu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 17

ذُرِّيَّةَ مَنۡ حَمَلۡنَا مَعَ نُوحٍۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَبۡدٗا شَكُورٗا

Enyi kizazi tuliyo wachukua pamoja na Nuhu! Hakika yeye alikuwa mja mwenye shukrani. info

Nyinyi Wana wa Israili mmezalikana kutokana na wale watu safi wema walio kuwa na Nuhu katika safina baada ya kuwa wameamini. Nasi tukawaokoa wasizame. Basi mfanyeni Nuhu kuwa ndiye mwongozi wenu wa kumfuata, kama walivyo mfanya wazee wenu walio tangulia. Kwani hakika yeye alikuwa mja wa wingi wa shukrani kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema zake.

التفاسير:

external-link copy
4 : 17

وَقَضَيۡنَآ إِلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ لَتُفۡسِدُنَّ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَرَّتَيۡنِ وَلَتَعۡلُنَّ عُلُوّٗا كَبِيرٗا

Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya fisadi katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa. info

Na tukatekeleza hukumu yetu kwa Wana wa Israili katika tuliyo yaandika katika Lauhun Mahfuudh, Ubao Ulio Hifadhiwa, ya kwamba watafanya ufisadi katika Nyumba Takatifu (Baitul Muqaddas) bila ya shaka yoyote mara mbili. Kila mara katika hizo itakuwa ni udhaalimu na uasi, na kuacha hukumu za Taurati, na kuwauwa Manabii, na mtasaidiana katika madhambi, na kwamba utawala wenu utaenea, na kutukuka na kupanda kichwa na kiburi kwa dhulma zenu.

التفاسير:

external-link copy
5 : 17

فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ أُولَىٰهُمَا بَعَثۡنَا عَلَيۡكُمۡ عِبَادٗا لَّنَآ أُوْلِي بَأۡسٖ شَدِيدٖ فَجَاسُواْ خِلَٰلَ ٱلدِّيَارِۚ وَكَانَ وَعۡدٗا مَّفۡعُولٗا

Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa. info

Na ulipo fika wakati wa kukuleteeni adhabu mara ya kwanza, tulikupatilizeni, kwa sababu ya fisadi yenu, kwa kukusalitishieni watu wa kali kupigana. Wakakuingilieni mpaka ndani ya majumba, hapana walicho kiacha, ili wakuuweni. Na ahadi ya kukuadhibuni ilikuwa ni ahadi haina budi kutimizwa.

التفاسير:

external-link copy
6 : 17

ثُمَّ رَدَدۡنَا لَكُمُ ٱلۡكَرَّةَ عَلَيۡهِمۡ وَأَمۡدَدۡنَٰكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَجَعَلۡنَٰكُمۡ أَكۡثَرَ نَفِيرًا

Kisha tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, na tukakusaidieni kwa mali na wana, na tukakujaalieni mkawa wengi zaidi. info

Kisha mambo yenu yalipo kaa sawa, na mkaongoka, na mkatengeneza umoja wenu, na mkaacha ufisadi, tukakurejezeeni ushindi juu ya wale makhasimu zenu. Nasi tukakuruzukuni mali na wana, na mkazidi kuwa wingi kwa idadi.

التفاسير:

external-link copy
7 : 17

إِنۡ أَحۡسَنتُمۡ أَحۡسَنتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡۖ وَإِنۡ أَسَأۡتُمۡ فَلَهَاۚ فَإِذَا جَآءَ وَعۡدُ ٱلۡأٓخِرَةِ لِيَسُـُٔواْ وُجُوهَكُمۡ وَلِيَدۡخُلُواْ ٱلۡمَسۡجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوۡاْ تَتۡبِيرًا

Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa. info

Na tukawambia: Mkifanya wema na mkamt'ii Mwenyezi Mungu, wema wenu utakufaeni nafsi zenu duniani na Akhera. Na mkifanya uovu kwa maasi, basi mnajiharibia nafsi zenu vile vile. Na utapo kuja wakati wa adhabu pale mara ya mwisho katika zile mara mbili za ufisadi wenu katika nchi, tutakupelekeeni maadui zenu, wafanye athari za uovu na madhila na huzuni zidhihiri nyusoni mwenu. Na matokeo yake ni kuingia katika Msikiti wa Baitul Muqaddas, wakauharibu kama walivyo ingia na wakauharibu mara ya kwanza, wakateketeza watacho kipata kwa uteketezi mkubwa.

التفاسير: