[1] Al-Bahira ni ngamia jike ambaye sikio lake hukatwa ikiwa atazaa idadi fulani ya ngamia, na As-Sa’iba ni ngamia jike ambaye anapofika umri fulani huachiwa masanamu yao, na Al-Wasiila ni ngamia jike anayezaa jike baada ya jike mwingine, na Al-Haami ni ngamia dume ambaye watazalishwa idadi fulani ya ngamia kutoka kwa mgongo wake. (Al-Mukhtaswar fit-tafsiir)