വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

external-link copy
216 : 2

كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡقِتَالُ وَهُوَ كُرۡهٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـٔٗا وَهُوَ شَرّٞ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ

Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinawachukiza. Lakini huenda mkachukia kitu, nacho ni heri kwenu. Na huenda mkapenda kitu, nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.[1] info

[1] Kuchukia huku kunahusiana na maumbile, ambayo kawaida hayalipendi kwa sababu ya yale yaliyomo ndani yake kama vile kutoa mali, na ugumu juu ya nafsi, na kuhatarisha nafsi. Na siyo kwa sababu ya kuichukia amri ya Mwenyezi Mungu. (Tafsir Al-Baghawi)

التفاسير: