വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

external-link copy
197 : 2

ٱلۡحَجُّ أَشۡهُرٞ مَّعۡلُومَٰتٞۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ ٱلۡحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي ٱلۡحَجِّۗ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ يَعۡلَمۡهُ ٱللَّهُۗ وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيۡرَ ٱلزَّادِ ٱلتَّقۡوَىٰۖ وَٱتَّقُونِ يَٰٓأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Hijja ni miezi maalumu. Basi anayehirimia Hijja ndani yake (miezi hiyo), basi asijamiiane wala asipindukie mipaka wala asibishane katika Hijja. Na chochote mnachokifanya katika heri, Mwenyezi Mungu anaijua. Na chukueni masurufu. Na hakika, masurufu (yaliyo) bora zaidi ni uchamungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili na busara! info
التفاسير: