വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

external-link copy
156 : 2

ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٞ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٰجِعُونَ

Wale ambao ukiwapata msiba, husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.[1] info

[1] Wao husema hivyo kwa sababu wanajua kwamba wanamilikiwa na Mwenyezi Mungu, wanasimamiwa chini ya amri yake na uendeshaji wake. Kwa hivyo, hatuna chochote katika nafsi zetu wala mali zetu. Na akitujaribu kwa kitu katika hayo, basi Yeye Mwingi wa Rehema atakuwa amewaendesha wamilikiwa wake na mali zake. Kwa hivyo haifai kuwa na pingamizi lolote dhidi yake. (Tafsir Assa'dii)

التفاسير: