വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

external-link copy
154 : 2

وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٰتُۢۚ بَلۡ أَحۡيَآءٞ وَلَٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ

Wala msiseme kuwa wale waliouwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti. Bali hao ni hai. Lakini nyinyi hamtambui.[1] info

[1] Inajulikana kuwa kipenzi hakiachiwi na wenye akili timamu, isipokuwa kwa ajili ya kipenzi kilicho juu zaidi na kikubwa kukiliko. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuuawa katika njia yake akipigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, ili neno la Mwenyezi Mungu liwe ndilo la juu zaidi; na dini yake iwe iliyo dhahiri zaidi. Basi yeye kwa hakika hajakosa uhai alioupenda, bali (alipouawa) alipata uhai mkubwa na kamili zaidi kuliko mnavyofikiria nyinyi. (Tafsir Assa'dii)

التفاسير: