വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി വിവർത്തനം - റുവ്വാദ് തർജമ സെൻ്റർ

external-link copy
145 : 2

وَلَئِنۡ أَتَيۡتَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ بِكُلِّ ءَايَةٖ مَّا تَبِعُواْ قِبۡلَتَكَۚ وَمَآ أَنتَ بِتَابِعٖ قِبۡلَتَهُمۡۚ وَمَا بَعۡضُهُم بِتَابِعٖ قِبۡلَةَ بَعۡضٖۚ وَلَئِنِ ٱتَّبَعۡتَ أَهۡوَآءَهُم مِّنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلۡعِلۡمِ إِنَّكَ إِذٗا لَّمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na hata ukiwaletea hao waliopewa Kitabu hoja za kila namna, hawatafuata Kibla chako. Wala wewe hutafuata kibla chao. Wala baadhi yao hawatafuata kibla cha wengineo. Na kama ukiyafuata matamanio yao baada ya kile kilichokufikia katika elimu, wewe kwa hakika hapo utakuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.[1] info

[1] Hili linabainisha kumakinika kwao katika kufuata matamanio ya nafsi, na kwamba kuwahalifu huku wanakowahalifu na ukaidi wao sio dhidi yenu tu, bali hata hali yao wao kwa wao ni hivyo. (Tafsir Al-Alusi)

التفاسير: