വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

An-Nazi'at

external-link copy
1 : 79

وَٱلنَّٰزِعَٰتِ غَرۡقٗا

Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu! info

Ninaapa kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuving'oa vitu kutokana na pahala pao kwa nguvu,

التفاسير:

external-link copy
2 : 79

وَٱلنَّٰشِطَٰتِ نَشۡطٗا

Na kwa wanao toa kwa upole! info

Na kwa kila kilicho pewa uwezo wa kuvitoa vitu kwa utaratibu na ulaini,

التفاسير:

external-link copy
3 : 79

وَٱلسَّٰبِحَٰتِ سَبۡحٗا

Na wanao ogelea! info

Na kwa kila kilicho pewa mbio za kutekeleza kazi yake kwa sahala na wepesi.

التفاسير:

external-link copy
4 : 79

فَٱلسَّٰبِقَٰتِ سَبۡقٗا

Wakishindana mbio! info

Na kwa vinavyo shindania kutimiza waajibu ulio twikwa juu yao kushindania kwa juhudi,

التفاسير:

external-link copy
5 : 79

فَٱلۡمُدَبِّرَٰتِ أَمۡرٗا

Wakidabiri mambo. info

Na vinavyo dabiri, kupanga, mambo na kuyaendesha kwa mujibu wa vilivyo khusishwa,

التفاسير:

external-link copy
6 : 79

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلرَّاجِفَةُ

Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka! info

Bila ya shaka Saa ya Kiyama itafika; hiyo siku ambayo mpulizo wa mwanzo wa barugumu utavitikisa viumbe vyote,

التفاسير:

external-link copy
7 : 79

تَتۡبَعُهَا ٱلرَّادِفَةُ

Kifuate cha kufuatia. info

Na mpulizo huo utafuatiwa na wa pili ambao ndio utakao kuwa wa kufufuliwa watu.

التفاسير:

external-link copy
8 : 79

قُلُوبٞ يَوۡمَئِذٖ وَاجِفَةٌ

Siku hiyo nyoyo zitapiga piga! info

Siku hiyo nyoyo zitapapatika kwa khofu.

التفاسير:

external-link copy
9 : 79

أَبۡصَٰرُهَا خَٰشِعَةٞ

Macho yatainama chini! info

Macho ya watu yatakuwa na huzuni, manyonge.

التفاسير:

external-link copy
10 : 79

يَقُولُونَ أَءِنَّا لَمَرۡدُودُونَ فِي ٱلۡحَافِرَةِ

Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? info

Watu hawa husema duniani kwa kukanya kufufuliwa: Ati tutarudishwa sisi baada ya kwisha kufa, tuumbwe tena kama tulivyo kuwa?

التفاسير:

external-link copy
11 : 79

أَءِذَا كُنَّا عِظَٰمٗا نَّخِرَةٗ

Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? info

Tukisha kuwa mafupa yaliyo chakaa, ati tutarejeshwa tufufuliwe upya?

التفاسير:

external-link copy
12 : 79

قَالُواْ تِلۡكَ إِذٗا كَرَّةٌ خَاسِرَةٞ

Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! info

Wanasema, kwa kukanya na kejeli: Kurejea huko kama kukitokea basi ni marejeo ya khasara, na sisi si watu wa kukhasiri.

التفاسير:

external-link copy
13 : 79

فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ

Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, info

Msidhani kurejea huko ni kuzito. Kwani hayo ni ukelele mmoja tu,

التفاسير:

external-link copy
14 : 79

فَإِذَا هُم بِٱلسَّاهِرَةِ

Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! info

Mara maiti wote watahudhurishwa kwenye ardhi ya mkusanyiko!

التفاسير:

external-link copy
15 : 79

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ

Je! Imekufikia hadithi ya Musa? info

Ewe Muhammad! Imekufikilia hadithi ya Musa,

التفاسير:

external-link copy
16 : 79

إِذۡ نَادَىٰهُ رَبُّهُۥ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوًى

Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: info

Alipo mwita Mola wake Mlezi katika bonde lilio takaswa, linalo itwa "T'uwa"?

التفاسير: