വിശുദ്ധ ഖുർആൻ പരിഭാഷ - സവാഹിലി പരിഭാഷ - അലി മുഹ്സിൻ അൽബർവാനി

An-Naba

external-link copy
1 : 78

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ

WANAULIZANA nini? info

Wanaulizana nini hao makafiri?

التفاسير:

external-link copy
2 : 78

عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ

Ile khabari kuu! info

Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa,

التفاسير:

external-link copy
3 : 78

ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ

Ambayo kwayo wanakhitalifiana. info

Ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka.

التفاسير:

external-link copy
4 : 78

كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

La! Karibu watakuja jua. info

Kuwazuia kuulizana huko wanaambiwa kuwa watakuja ujua ukweli wa mambo hapo watapo ona kufufuliwa kumetokea khasa.

التفاسير:

external-link copy
5 : 78

ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Tena la! Karibu watakuja jua. info

Tena kuwazuia, watakuja jua itapo wateremkia adhabu.

التفاسير:

external-link copy
6 : 78

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا

kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko? info

Kwani wao hawaoni Ishara za uweza wetu kwamba Sisi tumeifanya ardhi imetandikwa upatikane utulivu juu yake na iwezekane kutembea juu yake?

التفاسير:

external-link copy
7 : 78

وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا

kama Na milima vigingi? info

Na tukaifanya milima ni vigingi vya ardhi vya kuituliza? Sehemu ya gamba gumu lilio juu ya ardhi linfikilia kiasi ya kilomita 60 unene wake, na inazidi mikunjo, mifimbi, inapanda juu kuwa milima, na huteremka chini kuwa ni vina vya bahari; na hiyo hulingana kwa sababu ya uzito unao patikana kutokana na milima. Na kulingana huko hakuharibiki ila kwa kubugunyika, kwani gamba kavu la ardhi linazuiliwa na milima, kama vigingi vinavyo zuilia khema. (Rejea Maoni ya Wataalamu juu ya Aya 7 ya Surat Qaf).

التفاسير:

external-link copy
8 : 78

وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا

Na tukakuumbeni kwa jozi? info

Na tukakuumbeni kwa jozi, wanaume na wanawake?

التفاسير:

external-link copy
9 : 78

وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا

Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? info

Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko ya machofu ya kazi? Kulala usingizi ni kusita nishat'i ya sehemu ya ubongo yenye kutambua na kuwa macho. Yaani gamba la ubongo, au kupunguka nishat'i yake kwa wingi, ukilinganisha na daraja za nishat'i ya sehemu za viungo vilio baki. Na kwa hivyo kunapunguka nguvu na joto la mwili, tena mwili hapo wakati wa usingizi hupata kutua na kupumzika baada ya kuhangaika viungo au akili au vyote viwili. Basi kazi za kimwili zote hupunguka isipo kuwa kazi za kusaga chakula, na kupitisha mkojo katika mafigo, na kutoka majasho katika ngozi, kwani yakisita hayo hupatikana madhara juu ya maisha ya mtu. Ama kuvuta pumzi huko nako hupunguka, na huwa ni kwa ndani zaidi, na huwa kwa kifua zaidi kuliko kwa tumbo. Na mpigo wa mishipa hupungua kasi kwa kunavyo tokana na moyo, na hudhoofika mkazano wa musulo (muscular tension), na kwa hivyo huwa taabu kupata harakati za kinyume. Na yote haya ni ili binaadamu apate kupumzika wakati wa kulala.

التفاسير:

external-link copy
10 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا

Na tukaufanya usiku ni nguo? info

Na tumeufanya usiku ni sitara kwenu kwa kiza kinacho kufunikeni.

التفاسير:

external-link copy
11 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا

Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? info

Na tumeufanya mchana ni wakati wa kuhangaika kwenu kutafuta cha kukusaidieni katika maisha yenu.

التفاسير:

external-link copy
12 : 78

وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا

Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? info

Na tumesimamisha juu yenu mbingu saba zenye nguvu madhubuti.

التفاسير:

external-link copy
13 : 78

وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا

Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; info

Na Sisi tumeliumba jua lenye mwangaza na linalo waka. Makusudio ya Assiraj Alwahhaaj, Taa yenye mwanga na joto, ni Jua. Na hayo kama ilivyo thibiti katika sayansi kuwa daraja ya joto la uso wake inafika daraja 6000. Ama kati yake daraja yake inazidi daraja 30 milioni kwa sababu ya mdidimizo mkubwa unao patikana juu ya madda ziliomo ndani yake. Na jua linatoa nishat'i hizi zifuatazo: 9 katika 100 ya miale ya Ultraviolet rays, 46 katika 100 ya miale ya mwangaza, 45 katika 100 miale ya joto, au Infra red rays. Na kwa hivyo hii Aya tukufu imeliita kuwa ni Taa yenye mwangaza na joto.

التفاسير:

external-link copy
14 : 78

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا

Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, info

Na tumeteremsha kutokana na mawingu yaliyo karibia kunyesha maji yenye kumiminika kwa nguvu. Mvua ndio kitu pekee kinacho toka asli yake maji matamu katika ardhi. Na asli ya mvua ni kukusanyika vijisehemu vya maji yanayo panda kutoka baharini, na maziwa na mito, yakakusanyika kama mawingu na yakageuka chembe za mvua au vipande vya barafu, na khatimaye yakaanguka kwa sura ya mvua au theluji.

التفاسير:

external-link copy
15 : 78

لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا

Ili tutoe kwayo nafaka na mimea. info

Ili tutoe kwa maji haya nafaka na mimea kuwa ni chakula kwa ajili ya watu na wanyama.

التفاسير:

external-link copy
16 : 78

وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا

Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. info

Na mabustani yenye miti iliyo fungamana na matawi yake yameingiliana.

التفاسير:

external-link copy
17 : 78

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا

Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, info

Hakika siku ya uamuzi baina ya viumbe imewekewa miadi ilio kwisha kadiriwa kwa ajili ya kufufuliwa.

التفاسير:

external-link copy
18 : 78

يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا

Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, info

Siku litakapo pulizwa barugumu na kufufuliwa watu, mtakuja kwenye mkutano makundi kwa makundi.

التفاسير:

external-link copy
19 : 78

وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا

Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango. info

Na mbingu zitapasuliwa kila upande hata zitakuwa ni milango milango.

التفاسير:

external-link copy
20 : 78

وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا

Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. info

Na milima itaondolewa baada ya kung'olewa mwahala mwake, na kuvurugwa, ikawa unaiona kama sura ya milima na hali hiyo ni kifusi tu kilicho rindikwa, kama uonavyo mangati, sarabi, unaona kama sura ya maji nayo si maji.

التفاسير:

external-link copy
21 : 78

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا

Hakika Jahannamu inangojea! info

Hakika Jahannamu imekuwa kama ni kitu kinacho ngojea, walinzi wake wanawangojea watu watakao kuja kuingia.

التفاسير:

external-link copy
22 : 78

لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا

Kwa walio asi ndio makaazi yao, info

Yawe ni marejeo na mafikio kwa wenye kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 78

لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا

Wakae humo karne baada ya karne, info

Watakaa humo dahari baada ya dahari.

التفاسير:

external-link copy
24 : 78

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا

Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, info

Hawataonja humo hata chembe ya upepo wa kuburudisha joto lake, wala kinywaji cha kupoza kiu chao.

التفاسير:

external-link copy
25 : 78

إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا

Ila maji yamoto sana na usaha, info

Lakini watakunywa maji yalio pita ukomo kwa umoto wake, na usaha unao miminika kutokana na ngozi za watu wa Motoni.

التفاسير:

external-link copy
26 : 78

جَزَآءٗ وِفَاقًا

Ndio jaza muwafaka. info

Malipo ya kuwafikiana na vitendo vyao viovu.

التفاسير:

external-link copy
27 : 78

إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا

Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. info

Kwani hao hawakutaraji kuwa itakuwapo kuhisabiwa, hata watende ya kuwaokoa humo.

التفاسير:

external-link copy
28 : 78

وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا

Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. info

Wakazikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha kufufuliwa kwa mkadhibisho mkali.

التفاسير:

external-link copy
29 : 78

وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا

Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. info

Na kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika.

التفاسير:

external-link copy
30 : 78

فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا

Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! info

Basi onjeni, wala hampati kwetu ila kuzidishiwa adhabu tu.

التفاسير:

external-link copy
31 : 78

إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا

Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, info

Hakika wenye kumcha Mola wao Mlezi watapata kuokoka na adhabu, na wataipata Pepo,

التفاسير:

external-link copy
32 : 78

حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا

Mabustani na mizabibu, info

Na mabustani yenye matunda, na mizabibu mizuri,

التفاسير:

external-link copy
33 : 78

وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا

Na wake walio lingana nao, info

Na wanawari walio watipwatipwa wa hirimu yao,

التفاسير:

external-link copy
34 : 78

وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا

Na bilauri zilizo jaa, info

Na bilauri safi zilizo jaa pomoni,

التفاسير:

external-link copy
35 : 78

لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّٰبٗا

Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo, info

Hawasikii huko Peponi upuuzi wala uwongo.

التفاسير:

external-link copy
36 : 78

جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا

Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. info

Ni malipo kutokana na Mola wako Mlezi, kwa fadhila yake na ihsani ya kutosha.

التفاسير:

external-link copy
37 : 78

رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! info

Mola Mlezi wa mbinguni na duniani na vilio baina yao, ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu. Hapana yeyote mwenye madaraka ya kusema mbele yake.

التفاسير:

external-link copy
38 : 78

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا

Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. info

Siku atakapo simama Jibrili na Malaika walio teuliwa nao wamenyenyekea, hasemi mmoja wao ila akipewa idhini na Arrahman, Mwingi wa rehema, kuwa aseme, naye atasema lilio sawa tu.

التفاسير:

external-link copy
39 : 78

ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا

Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi info

Hiyo ndiyo siku isiyo na shaka. Basi atakaye na ashike njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi arejee kwa Imani, na a'mali njema.

التفاسير:

external-link copy
40 : 78

إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا

Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! info

Hakika Sisi tumekuhadharisheni na adhabu itakayo tokea karibu, siku atakapo angalia mtu vitendo vyake vilivyo tangulizwa na mikono yake, na atakapo sema kafiri kwa kutamani kuokoka: Laiti ningeli bakia udongo baada ya kufa, nisifufuliwe wala nisihisabiwe!

التفاسير: