Walipo onana makundi mawili, watu wa Musa walisema: Hakika Firauni na watu wake watatupata. Basi tutaangamia.
Musa akasema: Hakika mimi ninao uangalizi wa Mwenyezi Mungu unao nifuata kwa kunihifadhi. Na Yeye ataniongoza kwenye Njia ya uwokovu. Amesema hayo ili awatuze kuwa watasalimika, na iwe mbali na mawazo yao fikra ya kutisha kwamba takuja patikana. .
Tukamuamrisha Musa kwa wahyi, ufunuo, aipige bahari kwa fimbo yake. Ikapasuka bahari njia kumi na mbili kwa mujibu wa idadi ya mataifa ya Wana wa Israili. Kila njia katika hizo njia ilikuwa na kizuizi cha maji yaliyo nyanyuka kama mlima ulio simama imara.
Hakika katika vituko hivi vya ajabu vya kiungu pana funzo la kuzingatia kwa atakaye kunafiika. Lakini watu wengi si wenye kusadiki.
Kwani hakika hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni maaadui kwangu mimi na kwenu. Basi mimi siwaabudu hao. Lakini ninaye muabudu na najijongeza kwake ni Muumba wa walimwengu wote, na Mwenye kumiliki mambo yao, na Mwenye kuwalinda.
Ibrahim a.s. akasema kwa kuomba: Mola wangu Mlezi! Nitunukie ukamilifu wa ilimu na vitendo, ili nipate kustahili kuubeba Ujumbe wako na hukummu kwa waja wako, na niwezeshe niungane pamoja na kundi la watendao wema.