Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Ali Muhsin Al-Barvani

Al-Mursalat

external-link copy
1 : 77

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا

Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole!  info

Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,

التفاسير:

external-link copy
2 : 77

فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا

Na zinazo vuma kwa kasi! info

Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,

التفاسير:

external-link copy
3 : 77

وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا

Na zikaeneza maeneo yote! info

Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,

التفاسير:

external-link copy
4 : 77

فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا

Na zinazo farikisha zikatawanya! info

Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,

التفاسير:

external-link copy
5 : 77

فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا

Na zinazo peleka mawaidha! info

Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,

التفاسير:

external-link copy
6 : 77

عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا

Kwa kuudhuru au kuonya, info

Ili iwe ni udhuru kwao na onyo wasiwe na hoja,

التفاسير:

external-link copy
7 : 77

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ

Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! info

Hakika haya mliyo ahidiwa ya kuja Kiyama kwa yakini yatatimia tu bila ya shaka yoyote.

التفاسير:

external-link copy
8 : 77

فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ

Wakati nyota zitakapo futwa, info

Basi nyota zitapo ondolewa kabisa,

التفاسير:

external-link copy
9 : 77

وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ

Na mbingu zitakapo pasuliwa, info

Na mbingu zitapo pasuka,

التفاسير:

external-link copy
10 : 77

وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ

Na milima itakapo peperushwa, info

Na milima ikavurugwa na ikapeperushiwa mbali na upepo,

التفاسير:

external-link copy
11 : 77

وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ

Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, info

Na Mitume wakawekewa wakati maalumu wahudhurie kwa ajili ya kuwatolea ushahidi kaumu zao.

التفاسير:

external-link copy
12 : 77

لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ

Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? info

Kwa ajili ya siku gani yametayarishwa mambo haya makubwa makubwa?

التفاسير:

external-link copy
13 : 77

لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ

Kwa siku ya kupambanua! info

Kwa ajili ya siku watakapo pambanuliwa baina ya viumbe.

التفاسير:

external-link copy
14 : 77

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ

Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? info

Na nini cha kukujuvya ina nini hiyo siku ya kupambanua?

التفاسير:

external-link copy
15 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! info

Ni maangamio ya milele siku hiyo kwa hao wanao kadhibisha walio waahidi Mitume!

التفاسير:

external-link copy
16 : 77

أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ

Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? info

Kwani hatukuwaangamiza mataifa ya zamani yaliyo kadhibisha,

التفاسير:

external-link copy
17 : 77

ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ

Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? info

Na kisha tukawafuatilizia hao wenginewe tukawateketeza hali kadhaalika,

التفاسير:

external-link copy
18 : 77

كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ

Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! info

Kwa madhambi waliyo yafanya na walivyo mkataa Mwenyezi Mungu?

التفاسير:

external-link copy
19 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Siku hiyo ni siku ya kuteketezwa walio kadhibisha, kama tulivyo waahidi.

التفاسير:

external-link copy
20 : 77

أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ

Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? info

Kwani hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili, nayo ni manii,

التفاسير:

external-link copy
21 : 77

فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ

Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? info

Na tukayaweka maji haya katika pahala patulivu,

التفاسير:

external-link copy
22 : 77

إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ

Mpaka muda maalumu? info

Mpaka kutimilia kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake kwa muda anao ujua Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
23 : 77

فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ

Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. info

Nasi tukaweka vipimo katika kuumbwa kwake, na kutengenezwa kwake, na kutoka kwake. Basi wabora wa kupima na kukadiria ni Sisi.

التفاسير:

external-link copy
24 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Ole wao hao wanao kadhibisha neema za kuumba na kukadiria.

التفاسير:

external-link copy
25 : 77

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا

Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya info

Kwani hatukuifanya ardhi kuwa imekusanya juu ya mgongo wake

التفاسير:

external-link copy
26 : 77

أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا

Walio hai na maiti? info

Viumbe vilivyo hai visio hisabika, na vilio kufa visio kadirika,

التفاسير:

external-link copy
27 : 77

وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا

Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? info

Na tukaweka milima iliyo thibiti imara mirefu, na tukakunywesheni maji matamu?

التفاسير:

external-link copy
28 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Wataangamia siku hiyo hao wanao kadhibisha neema hizi!

التفاسير:

external-link copy
29 : 77

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! info

Siku ya kupambanua wataambiwa makafiri: Nendeni huko Motoni mliko kuwa mkikukanusha.

التفاسير:

external-link copy
30 : 77

ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ

Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! info

Nendeni kwenye joto la moshi wa Jahannamu ulio gawika kwa ukubwa wake mapande matatu.

التفاسير:

external-link copy
31 : 77

لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ

Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. info

Hapana cha kujikinga na joto la siku hiyo, wala kivuli hicho hakipunguzi joto la mwako hata kidogo.

التفاسير:

external-link copy
32 : 77

إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ

Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! info

Moto huo hutupa macheche yenye ukubwa kama majumba,

التفاسير:

external-link copy
33 : 77

كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ

Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! info

Au utaona hayo macheche kama ngamia weusi wenye kuingia rangi ya manjano.

التفاسير:

external-link copy
34 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Wataangamia siku hiyo wanao kanusha kwamba hizi ndizo sifa za Moto.

التفاسير:

external-link copy
35 : 77

هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ

Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, info

Haya uliyo simuliwa yatatokea katika siku ambayo hawatatamka kitu cha kuwanufaisha,

التفاسير:

external-link copy
36 : 77

وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ

Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. info

Wala hawatakuwa na idhini ya kutamka, wala hawatatoa udhuru, kwani hawana udhuru.

التفاسير:

external-link copy
37 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! info

Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha siku hii.

التفاسير:

external-link copy
38 : 77

هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ

Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. info

Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,

التفاسير:

external-link copy
39 : 77

فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ

kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! info

Kama mnayo hila ya kujikinga na adhabu basi fanyeni hila hiyo. Basi njooni muepukane na adhabu yangu.

التفاسير:

external-link copy
40 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! info

Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha ahadi ya Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
41 : 77

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ

Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, info

Hakika wachamngu wenye kujikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika kivuli kikubwa, na chemchem zinazo miminika,

التفاسير:

external-link copy
42 : 77

وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ

Na matunda wanayo yapenda, info

Na matunda wanayo yaonea ladha, na wanayo yapenda,

التفاسير:

external-link copy
43 : 77

كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. info

Wataambiwa kwa kuamkiwa na kukirimiwa: Kuleni na mnywe chakula na vinywaji kwa starehe kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kuwa mkivitenda duniani.

التفاسير:

external-link copy
44 : 77

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. info

Hakika Sisi huwalipa mfano wa malipo hayo matukufu watu wema.

التفاسير:

external-link copy
45 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha Pepo.

التفاسير:

external-link copy
46 : 77

كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ

Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! info

Na makafiri wataambiwa: Kuleni na mjistareheshe kwa starehe isiyo baki muda mrefu, kwani hakika nyinyi ni wakosefu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
47 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Wataangamia siku hiyo wanao ikadhibisha neema.

التفاسير:

external-link copy
48 : 77

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ

Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. info

Na wakiambiwa: Swalini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mnyenyekeeni Yeye, hawanyenyekei wala hawaswali; bali hushikilia kiburi chao!

التفاسير:

external-link copy
49 : 77

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! info

Wataangamia siku wanao kadhibisha amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake.

التفاسير:

external-link copy
50 : 77

فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ

Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? info

Basi maneno gani hawa watayaamini ikiwa hawaiamini Qur'ani, na hali hii ni muujiza ulio toka mbinguni?

التفاسير: