Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Ali Muhsin Al-Barvani

Al-Humazah

external-link copy
1 : 104

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ

Ole wake kila safihi, msengenyaji! [1] info

[1] Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.

التفاسير:

external-link copy
2 : 104

ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ

Aliye kusanya mali na kuyahisabu. [2] info

[2] Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.

التفاسير:

external-link copy
3 : 104

يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ

Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! [3] info

[3] Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?

التفاسير:

external-link copy
4 : 104

كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ

Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. [4] info

[4] Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!

التفاسير:

external-link copy
5 : 104

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ

Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? [5] info

[5] Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?

التفاسير:

external-link copy
6 : 104

نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ

Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. [6] info

[6] Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa kwa amri yake, na daima unawaka!

التفاسير:

external-link copy
7 : 104

ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ

Ambao unapanda nyoyoni. [7] info

[7] Ambao unafikilia nyoyoni na kuzizunguka nyoyo.

التفاسير:

external-link copy
8 : 104

إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ

Hakika huo utafungiwa nao [8] info

[8] Huo utakuwa umefungwa milango yake, na wao watakuwa wamefungwa humo ndani

التفاسير:

external-link copy
9 : 104

فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ

Kwenye nguzo zilio nyooshwa. [9] info

[9] Kwenye maguzo yaliyo nyooka. Hawawezi kutaharaki, wala kutoka.

التفاسير: