Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

external-link copy
50 : 8

وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ يَتَوَفَّى ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَضۡرِبُونَ وُجُوهَهُمۡ وَأَدۡبَٰرَهُمۡ وَذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡحَرِيقِ

Na lau ingalionekana, ewe Mtume, hali ya Malaika ya kuzichukua roho za Makafiri na kuzitoa, na huku wao wanawapiga nyuso zao wakiwaelekea, na wanawapiga migongo yao wakiwakimbia na wanawaambia, «Onjeni adhabu inayounguza», ungaliona jambo kubwa. Na msururu huu wa maneno ingawa sababu yake ni vita vya Badr, lakini unakusanya hali ya kila kafiri. info
التفاسير: