Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Al-Muzzammil

external-link copy
1 : 73

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ

Ewe ulijifinika nguo zako! info
التفاسير:

external-link copy
2 : 73

قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا

Inuka uswali kipindi cha usiku isipokuwa sehemu chache yake. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 73

نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا

Inuka kwa muda wa nusu ya usiku au kupungua nusu kidogo mpaka ufikie theluthi. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 73

أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا

Au ongeza zaidi ya nusu mpaka ufikie theluthi mbili. Na usome Qur’ani kwa utaratibu na utulivu, uzifafanue herufi na vikomo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 73

إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا

Hakika sisi tutakuteremshia, ewe Nabii, Qur’ani tukufu inayokusanya maamrisho na makatazo na hukumu za kisheria. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 73

إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا

Hakika ibada inayo inayofanya ndani ya usiku ina athari kubwa zaid moyoni, na maneno yanabainika zaidi, kwa kuwa moyo uko mtupu hauna mashughuli ya kilimwengu. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 73

إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا

Hakika wewe katika kipindi cha mchana una wakati wa kuzunguka na kushughulika katika mambo yenye maslahi nawe na kufanya harakati nyingi kwa majukumu ya utume, basi wakati wa usiku ipe nafasi nafsi yako kumuabudu Mola wako. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 73

وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا

Na ulitaje, ewe Nabii, jina la Mola wako, umuombe kwalo na utindikie Kwake kikamilifu katika ibada yako na ujitegemeze Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 73

رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا

Yeye Ndiye Mmiliki wa Mashariki na Magharibi. Hakuna muabudiwa ka haki isipokuwa Yeye. Basi mtegemee Yeye na umuachie Yeye mambo yako. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 73

وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا

Na uvumilie kwa yale ambayo washirikina wanayasema kuhusu wewe na kuhusu Dini yako. Na uende kinyume na wao katika maneno yao ya ubatilifu pamoja na kuwapuuza na kuacha kuwalipiza. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 73

وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا

Na uniache mimi, ewe Mtume, na hawa wakanushaji wa aya zangu, wenye starehe na gogi la ulimwengu, na uwape muhula wa muda mchache kwa kucheleweshewa adhabu mpaka muda wa wao kuadhibiwa ufikie ukomo wake. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 73

إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا

Kwa hakika wao watapata kwetu sisi huko Akhera pingu nzito na Moto wenye kuwaka ambao watachomwa nao, info
التفاسير:

external-link copy
13 : 73

وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا

na chakula cha kuchukiza chenye kusakama kooni kisicho na ladha, na adhabu inayoumiza. info
التفاسير:

external-link copy
14 : 73

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا

Siku itakapotikisika na kusukikasukika ardhi na majabali mpaka majabali yawe mlima wa mchanga wenye kutiririka na kupeperuka, baada ya kuwa kwenye hali ya ugumu na ukavu. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 73

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا

Hakika sisi tumemtumiliza kwenu nyinyi, watu wa Makkah, Muhammad kuwa ni Mtume, mwenye kutoa ushahidi wa ukafiri na uasi unaotokana na nyinyi, kama vile tulivyomtumiliza Mūsā kuwa ni Mtume kwenda kwa Fir’awn aliyepita kiasi katika uasi. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 73

فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا

Basi Fir’awn akamkanusha Mūsā na asiukubali utume wake, na akakataa amri yake, tukamuangamiza maangamivu makali. Hapa pana onyo la kumuasi Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa kuogopea isije ikamfika yule aliyeasi mfano wa kile kilichomfika Fir‘awn na watu wake. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 73

فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا

Vipi mtajikinga nafsi zenu, mkikufuru, na adhabu ya Siku ya Kiyama ambayo huwafanya watoto wadogo watokwe na mvi kwa ukubwa wa janga lake na unguliko lake? info
التفاسير:

external-link copy
18 : 73

ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا

Mbingu zitakuwa na pasuko Siku hiyo, kwa ukubwa wa janga lake, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ya kuwa Siku hiyo itakuja ni yenye kutukia bila shaka. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 73

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا

Hakika aya hizi zenye kutisha ambazo ndani yake kuna vigongaji na vikemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea. info
التفاسير: