Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris: 142:128 close

external-link copy
119 : 6

وَمَا لَكُمۡ أَلَّا تَأۡكُلُواْ مِمَّا ذُكِرَ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَقَدۡ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيۡكُمۡ إِلَّا مَا ٱضۡطُرِرۡتُمۡ إِلَيۡهِۗ وَإِنَّ كَثِيرٗا لَّيُضِلُّونَ بِأَهۡوَآئِهِم بِغَيۡرِ عِلۡمٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُعۡتَدِينَ

Na kitu gani kinachowazuia, enyi Waislamu, kumla mnyama ambaye jina la Mwenyezi Mungu lilitajwa wakati wa kuchinjwa, ambapo Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Amewaelezea nyinyi yote aliyoyaharamisha kwenu? Lakini yale ya haramu ambayo dharura imepelekea yatumiwe, kwa sababu ya njaa, kama mfu, basi mumehalalishiwa. Na wengi, kati ya wapotofu, wanawapoteza wafuasi wao na kuwaepusha na njia ya Mwenyezi Mungu katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali kwa matakwa yao kwa ujinga walionao. Kwa hakika, Mola wako, ewe Mtume, Ndiye Amjuwaye zaidi yule aliyekiuka mipaka Yake katika hayo; na Yeye Ndiye Atakayesimamia hesabu yake na malipo yake. info
التفاسير:

external-link copy
120 : 6

وَذَرُواْ ظَٰهِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَبَاطِنَهُۥٓۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡسِبُونَ ٱلۡإِثۡمَ سَيُجۡزَوۡنَ بِمَا كَانُواْ يَقۡتَرِفُونَ

Na acheni, enyi watu, maasia yote, yaliyo waziwazi na yaliyo ya siri. Hakika wale wanaofanya maasia, Mola wao Atawatesa kwa sababu ya yale maovu ambyo walikuwa wakiyafanya. info
التفاسير:

external-link copy
121 : 6

وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ

Na wala msile, enyi Waislamu, katika vichinjwa, yule ambaye halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinjwa, kama mfu na aliochinjiwa masanamu na majini na wasiokuwa hao. Na kwa hakika kuwala wanyama hao ni kutoka kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Na majini waasi wanawatia marafiki zao, miongoni mwa mashetani wa kibinadamu, ushawiwishi wa kuwatatiza kuhusu uharamu wa kula mfu; wanawaamrisha wawaambie Waislamu wanapobishana nao, «Hakika nyinyi, kwa kutokula kwenu mfu, huwa hamli anachokiua Mwenyezi Mungu, ambapo mnakula mnachokichinja.» Na iwapo mtawasikiliza, enyi Waislamu, katika kuhalalisha mfu, basi nyinyi mtakuwa sawa na wao katika ushirikina. info
التفاسير:

external-link copy
122 : 6

أَوَمَن كَانَ مَيۡتٗا فَأَحۡيَيۡنَٰهُ وَجَعَلۡنَا لَهُۥ نُورٗا يَمۡشِي بِهِۦ فِي ٱلنَّاسِ كَمَن مَّثَلُهُۥ فِي ٱلظُّلُمَٰتِ لَيۡسَ بِخَارِجٖ مِّنۡهَاۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلۡكَٰفِرِينَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Je, yule ambaye amekufa katika upotofu, ameangamia na ameshangaa, tukaufufua moyo wake kwa Imani, tukamuongoza kwenye Imani na tukamuafikia kuwafuata Mitume Wake, akawa anaishi kwenye miangaza ya uongofu, atakuwa ni kama mfano wa yule aliye ndani ya ujinga, matamanio ya moyo na namna mbalimbali za upotevu, asiyeongokewa kwenye sehemu yoyote ya kupenya na hana wa kumuokoa na yale ambayo yumo ndani yake? Hao wawili hawalingani. Na kama nilivyomuachilia kafiri huyu anayebishana na nyinyi, enyi Waumini, nikampambia vitendo vyake viovu akaviona ni vyema, vilevile nimewapambia wenye kukanusha vitendo vyao viovu ili wapaswe, kwa hilo, kupata adhabu. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 6

وَكَذَٰلِكَ جَعَلۡنَا فِي كُلِّ قَرۡيَةٍ أَكَٰبِرَ مُجۡرِمِيهَا لِيَمۡكُرُواْ فِيهَاۖ وَمَا يَمۡكُرُونَ إِلَّا بِأَنفُسِهِمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Na mfano huu uliopatikana kwa viongozi wa makafiri huko Maka wa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, tumeweka katika kila mji watu waovu wanaongozwa na wakubwa wao, ili wapate kufanya vitimbi humo kwa kuzuia dini ya Mwenyezi Mungu; na wao hawazifanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao, na wala hawalihisi hilo. info
التفاسير:

external-link copy
124 : 6

وَإِذَا جَآءَتۡهُمۡ ءَايَةٞ قَالُواْ لَن نُّؤۡمِنَ حَتَّىٰ نُؤۡتَىٰ مِثۡلَ مَآ أُوتِيَ رُسُلُ ٱللَّهِۘ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ حَيۡثُ يَجۡعَلُ رِسَالَتَهُۥۗ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ صَغَارٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعَذَابٞ شَدِيدُۢ بِمَا كَانُواْ يَمۡكُرُونَ

Na pindi inapowajia washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Maka, hoja iliyo waziwazi juu ya unabii wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wanasema baadhi ya wakubwa wao, «Kamwe hatutaukubali unabii wake mpaka Mwenyezi Mungu Atupe unabii na miujiza mfano wa Aliyowapa wajumbe wake waliotangulia» Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Aliwajibu kwa neno lake,: “Mwenyezi Mungu Anajua zaidi wapi Auweke ujumbe Wake.» Kwa maana kuwa Anawajua wale wanaofaa kubeba ujumbe Wake na kuufikisha kwa Watu. Utawapata unyonge wakiukaji mipaka hawa, na watakuwa na adhabu iumizayo ndani ya Moto wa Jahanamu kwa sababu ya vitimbi vyao kwa Uislamu na watu wake. info
التفاسير: