Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris: 48:2 close

external-link copy
283 : 2

۞ وَإِن كُنتُمۡ عَلَىٰ سَفَرٖ وَلَمۡ تَجِدُواْ كَاتِبٗا فَرِهَٰنٞ مَّقۡبُوضَةٞۖ فَإِنۡ أَمِنَ بَعۡضُكُم بَعۡضٗا فَلۡيُؤَدِّ ٱلَّذِي ٱؤۡتُمِنَ أَمَٰنَتَهُۥ وَلۡيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥۗ وَلَا تَكۡتُمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَۚ وَمَن يَكۡتُمۡهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٞ قَلۡبُهُۥۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ عَلِيمٞ

Na mkiwa muko safarini, na msipate mwenye kuwaandikia, mpatieni yule mwenye haki kitu kiwe ni dhamana ya haki yake hadi mdaiwa atakapolipa deni yake. Na iwapo nyinyi kwa nyinyi mumeaminiana, hapana makosa kuacha kuandika, kushuhudisha na kuweka rahani, na deni itabaki ni amana kwenye shingo ya mdaiwa, ni juu yake kuilipa. Na ni juu yake amchunge Mwenyezi Mungu asimfanyiye hiana mwenzake. Na akikataa mdaiwa deni iliyo juu yake, na ikawa pana mtu aliyekuweko na kushuhudia, huyo itamlazimu kuutoa wazi ushahidi wake. Na mwenye kuuficha ushahudi huu, ni mtu mwenye moyo wa hiana na urongo. Na Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuchungulia siri zote, Ndiye Ambaye ujuzi Wake umezunguka mambo yenu yote, na Atawahesabu kwa hayo. info
التفاسير:

external-link copy
284 : 2

لِّلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَإِن تُبۡدُواْ مَا فِيٓ أَنفُسِكُمۡ أَوۡ تُخۡفُوهُ يُحَاسِبۡكُم بِهِ ٱللَّهُۖ فَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, kwa kuvimiliki, kuvipekesha na kuvijua. Hakuna chochote kinachofichika Kwake. Na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu Anakijua, na Atawahesabu nacho. Atamsamehe Anayemtaka na Atampatiliza Anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu. Baadaye Mwenyezi Mungu aliwakirimu Waislamu Akasamehe maneno ya mtu kuiyambia nafsi yake na mawazo ya moyo, yakiwa hayatafuatiwa na maneno au vitendo, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
285 : 2

ءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّن رُّسُلِهِۦۚ وَقَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَاۖ غُفۡرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake aiyakinishe. Na Waumini pia wameamini na kufanya amali zinazoambatana na Qur’ani Tukufu. Kila mmoja katika wao amemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Mwenyezi Mungu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako, Peke Yako, ndio marejeo yetu na mwisho wetu.» info
التفاسير:

external-link copy
286 : 2

لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَهَا مَا كَسَبَتۡ وَعَلَيۡهَا مَا ٱكۡتَسَبَتۡۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذۡنَآ إِن نَّسِينَآ أَوۡ أَخۡطَأۡنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تَحۡمِلۡ عَلَيۡنَآ إِصۡرٗا كَمَا حَمَلۡتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِنَاۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلۡنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦۖ وَٱعۡفُ عَنَّا وَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَآۚ أَنتَ مَوۡلَىٰنَا فَٱنصُرۡنَا عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Dini ya Mwenyezi Mungu ni sahali, haina uzito ndani yake. Mwenyezi Mungu hawatakii waja Wake wasiyoyaweza. Mwenye kufanya uzuri atapata uzuri, na mwenye kufanya ubaya atapata ubaya. Ewe Mola wetu! Usitutese tukisahau chochote miongoni mwa vitu ulivyotufaradhia au tukikosea kwa kufanya kitu chochote ulichotukataza kukifanya. Ewe Mola wetu! Na usitukalifishe kufanya matendo magumu uliyowakalifisha waliokuwa kabla yetu, miongoni mwa waasi, yakiwa ni mateso kwao. Ewe Mola wetu! Na usitubebeshe tusiyoyaweza ya amri ngumu na mikasa. Na uyafute madhambi yetu, uzisitiri aibu zetu na utufanyiwe wema. Wewe Ndiye Mwenye kuyamiliki mambo yetu na kuyaendesha. Tunusuru juu ya wale waliokataa Dini yako na kuukataa umoja wako na wakamkanusha Nabii wako Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, Na ujaalie mwisho mwema uwe ni wetu juu yao, ulimenguni na Akhera. info
التفاسير: