Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Vertimas į suahilių k. - Abdullah Muchamed ir Nasir Khamis

Puslapio numeris:close

external-link copy
43 : 13

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَسۡتَ مُرۡسَلٗاۚ قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ وَمَنۡ عِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡكِتَٰبِ

Na wenye kumkanusha Nabii wa Mwenyezi Mungu wanasema, «Ewe Muhammad, hukutumilizwa na Mwenyezi Mungu.» Waambie, «Inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni shahidi juu ya ukweli wangu na urongo wenu, na unatosha ushahidi wa wenye ujuzi wa Kitabu miongoni mwa Mayahudi na Wanaswara kati ya wale waliouamini utume wangu na kwamba yale niliokuja nayo yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na akaufuata ukweli na akatoa ushahidi huo waziwazi na asiufiche. info
التفاسير: