Ewe Nabii! Wakikujia wanawake Waumini kukuahidi kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatwauwa watoto wao, wala hawatawabandikiza waume zao watoto wao (wa haramu) kwa uzushi na uwongo wanao uzua baina ya mikono yao na miguu yao. (yaani matumboni mwao, au kwa ndimi zao na tupu zao); wala hawendi kinyume nawe katika jambo jema unalo waitia, basi pokea ahadi zao juu ya hayo, na waombee msamaha kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe na kurehemu. (Mtume s.a.w. haamrishi ila jema, lakini sharia hapo inasema kuwa mtawala yeyote hut'iiwa akiamrisha jema tu. Ama kwa lilio ovu, Mtume s.a.w. amesema: "Hapana kumtii kiumbe katika kumuasi Muumba.")
Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake, msiwafanye kuwa rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewaghadhibikia. Hao wamekata tamaa na Akhera na yote yatakao kuwapo huko, ya kulipwa na kuhisabiwa, kama makafiri walivyo kata tamaa kufufuliwa waliomo makaburini.