وه‌رگێڕانی ماناكانی قورئانی پیرۆز - وەرگێڕاوی سواحیلی - علی محسن البرواني

external-link copy
112 : 5

إِذۡ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ هَلۡ يَسۡتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِۖ قَالَ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. info

Ewe Nabii! Taja pia yaliyo tokea pale wafuasi wa Isa wenye ikhlasi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Hivyo Mola wako Mlezi atakuitikia ukimtaka akuteremshie chakula kutoka mbinguni? Isa akawaambia kuwajibu: Kama nyinyi ni kweli mnamuamini Mwenyezi Mungu, basi mkhofuni Yeye, na fuateni amri zake na makatazo yake. Wala msitafute hoja ila nilizo kuleteeni.

التفاسير: