وه‌رگێڕانی ماناكانی قورئانی پیرۆز - وەرگێڕاوی سواحیلی - عبد الله محمد و ناصر خميس

At-Talaq

external-link copy
1 : 65

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحۡصُواْ ٱلۡعِدَّةَۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ رَبَّكُمۡۖ لَا تُخۡرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخۡرُجۡنَ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُۥۚ لَا تَدۡرِي لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحۡدِثُ بَعۡدَ ذَٰلِكَ أَمۡرٗا

Ewe Mtume! Pindi mnapotaka, wewe na Waumini, kuwapa talaka wake zenu, basi wapeni talaka wakiwa kwenye hali ya kukabili kipindi cha wao kukaa eda- yaani kwenye hali ya usafi ambao hakukupatikana kuingiliwa, au katika hali ya mimba iliyo wazi- na mshike hesabu ya eda, mpate kujua muda wa kuwarejea iwapo mtataka kuwarejea, na muogopeni Mwenyezi Mungu, Mola wenu. Wala msiwatoe wanawake waliopewa talaka kwenye majumba wanayokaa mpaka eda lao limalizike, nalo ni hedhi tatu kwa asiyekuwa mdogo (asiyeingia damuni) na si kwa aliyekata tamaa ya kuingia damuni (kwa uzee) wala mwenye mimba. Na haifai kwa wanawake hao kutoka majumbani mwao wao wenyewe isipokuwa watakapofanya kitendo kiovu cha waziwazi kama vile uzinifu. Na hizo ndizo hukumu za Mwenyezi Mungu alizozipitisha kwa waja Wake. Na Mwenye kuzikiuka hukumu za Mwenyezi Mungu, basi huyo amejidhulimu nafsi yake na ameipeleka mahali pa maangamivu. Hujui, ewe mtoaji talaka, kwamba Mwenyezi Mungu huenda, baada ya talaka hiyo, Akaleta jambo usilolitazamia ukaja ukamrudia. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 65

فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمۡسِكُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ فَارِقُوهُنَّ بِمَعۡرُوفٖ وَأَشۡهِدُواْ ذَوَيۡ عَدۡلٖ مِّنكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلشَّهَٰدَةَ لِلَّهِۚ ذَٰلِكُمۡ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مَخۡرَجٗا

Na pindi kipindi cha eda la wanawake waliopewa talaka kinapokaribia kumalizika, basi warudieni na mtangamane nao kwa wema pamoja na kuwapatia matumizi, au waacheni pamoja na kuwatekelezea haki zao bila kuwafanyia mambo ya kuwadhuru. Na wekeni mashahidi mnaporejeana na mnapoachana, wanaume wawili waadilifu miongoni mwenu. Na tekelezeni, enyi mashahidi, ushahidi wenu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na sio kwa kitu kingine. Hilo ambalo Mwenyezi Mungu Amewaamrisha kwalo yuwawaidhiwa nalo yule anayemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na yoyote atakayemuogopa Mwenyezi Mungu akayafuata kivitendo yale ambayo Amemuamrisha nayo na akayaepuka yale ambayo Amemkataza nayo, Atamtolea njia ya kutoka kwenye kila dhiki info
التفاسير:

external-link copy
3 : 65

وَيَرۡزُقۡهُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَحۡتَسِبُۚ وَمَن يَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِ فَهُوَ حَسۡبُهُۥٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَٰلِغُ أَمۡرِهِۦۚ قَدۡ جَعَلَ ٱللَّهُ لِكُلِّ شَيۡءٖ قَدۡرٗا

na Atamfanyia nyepesi njia za kupata riziki kwa namna ambayo haikupita akilini mwake wala haikuwa kwenye hesabu zake. Na yoyote atakayemtegemea Mwenyezi Mungu basi Yeye Atamtosheleza yale yanayomkera katika mambo yake yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kulifikilia jambo Lake, Hapitwi na kitu chochote wala haelemewi na kitu chochote kinachotakikana na Yeye, hakika Mwenyezi Mungu Amekiwekea kila kitu muda wake wa kukomea na kipimo ambacho kitu hiko hakiwezi kukipita. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 65

وَٱلَّٰٓـِٔي يَئِسۡنَ مِنَ ٱلۡمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمۡ إِنِ ٱرۡتَبۡتُمۡ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَٰثَةُ أَشۡهُرٖ وَٱلَّٰٓـِٔي لَمۡ يَحِضۡنَۚ وَأُوْلَٰتُ ٱلۡأَحۡمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّهُۥ مِنۡ أَمۡرِهِۦ يُسۡرٗا

Na wanawake walioachwa ambao damu zao za hedhi zimekatika kwa utu uzima wao, mkitatizika mkawa hamjui: ni nini hukumu yao? Basi, eda lao ni miezi mitatu. Na wanawake wadogo ambao hawajaingia damuni, basi eda lao ni miezi mitatu vilevile. Na wanawake wajawazito, eda lao ni linamalizikia pale wanapozaa. Na yoyote atakayemuogopa mwenyezi Mungu na akatekeleza hukumu Zake, Atamfanyia mambo Yake yawe mepesi duniani na Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 65

ذَٰلِكَ أَمۡرُ ٱللَّهِ أَنزَلَهُۥٓ إِلَيۡكُمۡۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُعۡظِمۡ لَهُۥٓ أَجۡرًا

Hayo yailotajwa kuhusiana na mambo ya talaka na eda ni amri ya Mwenyezi Mungu Aliyoiteremsha kwenu, enyi watu, ili muitumie. Na yoyote mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu akawa anamcha kwa kuyaepuka yale ya kumuasi na kuzitekeleza faradhi Zake, basi Atamfutia madhambi yake, Atamuongezea kwa wingi malipo yake huko Akhera na amuingize Peponi. info
التفاسير: