وه‌رگێڕانی ماناكانی قورئانی پیرۆز - وەرگێڕاوی سواحیلی - عبد الله محمد و ناصر خميس

Al-Kafirun

external-link copy
1 : 109

قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ

Sema, ewe Mtume, kuwaambia waliokufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake: «Enyi wenye kumkanusha Mwenyezi Mungu! info
التفاسير:

external-link copy
2 : 109

لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ

«Mimi siabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 109

وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ

«Wala nyinyi si wenye kuabudu Mola Mmoja ninayemuabudu Ambaye ndiye Anayestahiki kuabudiwa. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 109

وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ

«Wala mimi si mwenye kuabudu mnavyoviabudu miongoni mwa masanamu na waungu wa urongo. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 109

وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ

«Wala nyinyi si wenye kuabudu mbeleni ninayemuabudu.» Aya hii imeteremka juu ya watu makhsusi miongoni mwa washirikina ambao Mwenyezi Mungu Alijua kuwa hawataamini kabisa. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 109

لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِيَ دِينِ

«Nyinyi mna dini yenu mnayoiamini na mimi nina Dini yangu ambayo sitaki nyingine.» info
التفاسير: