ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
119 : 16

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَ وَأَصۡلَحُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٌ

Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa wale waliotenda mabaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mazuri; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. info
التفاسير:

external-link copy
120 : 16

إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةٗ قَانِتٗا لِّلَّهِ حَنِيفٗا وَلَمۡ يَكُ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
121 : 16

شَاكِرٗا لِّأَنۡعُمِهِۚ ٱجۡتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ

Mwenye kuzishukuru neema zake. Yeye alimteua, na akamwongoa kwenye Njia iliyonyooka. info
التفاسير:

external-link copy
122 : 16

وَءَاتَيۡنَٰهُ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَإِنَّهُۥ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na tukampa mazuri katika dunia, naye hakika Akhera atakuwa miongoni mwa walio wema. info
التفاسير:

external-link copy
123 : 16

ثُمَّ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ أَنِ ٱتَّبِعۡ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
124 : 16

إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبۡتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحۡكُمُ بَيۡنَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Hakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa wale waliohitalifiana kuhusiana nayo. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Qiyama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana. info
التفاسير:

external-link copy
125 : 16

ٱدۡعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلۡحِكۡمَةِ وَٱلۡمَوۡعِظَةِ ٱلۡحَسَنَةِۖ وَجَٰدِلۡهُم بِٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ

Lingania kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri zaidi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea Njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka. info
التفاسير:

external-link copy
126 : 16

وَإِنۡ عَاقَبۡتُمۡ فَعَاقِبُواْ بِمِثۡلِ مَا عُوقِبۡتُم بِهِۦۖ وَلَئِن صَبَرۡتُمۡ لَهُوَ خَيۡرٞ لِّلصَّٰبِرِينَ

Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri. info
التفاسير:

external-link copy
127 : 16

وَٱصۡبِرۡ وَمَا صَبۡرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَلَا تَكُ فِي ضَيۡقٖ مِّمَّا يَمۡكُرُونَ

Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Wala usiwahuzunikie, wala usiwe katika dhiki kwa njama wanazozifanya. info
التفاسير:

external-link copy
128 : 16

إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ

Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na wale watendao mazuri. info
التفاسير: