ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
94 : 16

وَلَا تَتَّخِذُوٓاْ أَيۡمَٰنَكُمۡ دَخَلَۢا بَيۡنَكُمۡ فَتَزِلَّ قَدَمُۢ بَعۡدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُواْ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَكُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Wala msifanye viapo vyenu kuwa njia ya kudanganyana baina yenu, mguu ukaja teleza baada ya kuwa thabiti, na mkaonja mabaya kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu Njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa. info
التفاسير:

external-link copy
95 : 16

وَلَا تَشۡتَرُواْ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ ثَمَنٗا قَلِيلًاۚ إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua. info
التفاسير:

external-link copy
96 : 16

مَا عِندَكُمۡ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٖۗ وَلَنَجۡزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓاْ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mlivyo navyo vitakwisha, na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
97 : 16

مَنۡ عَمِلَ صَٰلِحٗا مِّن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَنُحۡيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةٗ طَيِّبَةٗۖ وَلَنَجۡزِيَنَّهُمۡ أَجۡرَهُم بِأَحۡسَنِ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, hakika tutamhuisha uhai mwema, na hakika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda. info
التفاسير:

external-link copy
98 : 16

فَإِذَا قَرَأۡتَ ٱلۡقُرۡءَانَ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

Na unaposoma Qur-ani, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na Shetani aliyelaaniwa. info
التفاسير:

external-link copy
99 : 16

إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. info
التفاسير:

external-link copy
100 : 16

إِنَّمَا سُلۡطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوۡنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشۡرِكُونَ

Hakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, na wale wanaofanya ushirika naye. info
التفاسير:

external-link copy
101 : 16

وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ

Na tunapobadilisha Ishara pahala pa Ishara, na Mwenyezi Mungu anayajua anayoyateremsha, wanasema: Wewe si chochote ila ni mzushi tu, lakini wengi wao hawajui tu. info
التفاسير:

external-link copy
102 : 16

قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ

Sema: Ameiteremsha Roho mtakatifu kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa haki, ili awaimarishe wale walioamini, na kuwa ni uwongofu, na bishara kwa Waislamu. info
التفاسير: