ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
57 : 39

أَوۡ تَقُولَ لَوۡ أَنَّ ٱللَّهَ هَدَىٰنِي لَكُنتُ مِنَ ٱلۡمُتَّقِينَ

Au ikasema: Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa wenye kumchamngu. info

Au iseme ile nafsi yenye dhambi, kutafuta udhuru: Lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli niwezesha kufuata uwongofu bila ya shaka ningeli kuwa duniani katika wale walio jilinda na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa Imani na vitendo vyema.

التفاسير:

external-link copy
58 : 39

أَوۡ تَقُولَ حِينَ تَرَى ٱلۡعَذَابَ لَوۡ أَنَّ لِي كَرَّةٗ فَأَكُونَ مِنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ

Au ikasema inapo ona adhabu: Lau kuwa ningeli pata fursa nyengine, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema. info

Au iseme nafsi ile yenye dhambi itapo ona adhabu: Laiti ningeli rejeshwa duniani, nikawa katika wanao tengeneza imani yao na vitendo vyao!

التفاسير:

external-link copy
59 : 39

بَلَىٰ قَدۡ جَآءَتۡكَ ءَايَٰتِي فَكَذَّبۡتَ بِهَا وَٱسۡتَكۡبَرۡتَ وَكُنتَ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Wapi! Bila ya shaka zilikujia Ishara zangu, nawe ukazikadhibisha, na ukajivuna, na ukawa miongoni mwa makafiri! info

Utayapata wapi, ewe mwenye majuto! Mafunzo yangu yalikujia katika ndimi za Mitume, nawe ukayakanusha, na ukajiona bora, ukakataa kuyafuata, na ukawa katika dunia yako miongoni mwa wenye kushikilia ukafiri.

التفاسير:

external-link copy
60 : 39

وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ تَرَى ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَى ٱللَّهِ وُجُوهُهُم مُّسۡوَدَّةٌۚ أَلَيۡسَ فِي جَهَنَّمَ مَثۡوٗى لِّلۡمُتَكَبِّرِينَ

Na Siku ya Kiyama utawaona walio msingizia uwongo Mwenyezi Mungu nyuso zao zimesawijika. Je! Si katika Jahannamu makaazi ya wanao takabari? info

Na Siku ya Kiyama utawaona walio mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, wakamkhusisha yasiyo kuwa yake, nyuso zao zimesawjika kwa huzuni na majonzi. Hakika Jahannamu ndio makaazi ya wenye kiburi wakaikataa Haki.

التفاسير:

external-link copy
61 : 39

وَيُنَجِّي ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ بِمَفَازَتِهِمۡ لَا يَمَسُّهُمُ ٱلسُّوٓءُ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ

Na Mwenyezi Mungu atawaokoa wenye kujikinga kwa ajili ya kufuzu kwao. Hapana uovu utao wagusa, wala hawatahuzunika. info

Na Mwenyezi Mungu atawaokoa alio wajaalia ulinzi isiwapate adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa vile alivyo kwisha wajua kuwa wamefuzu, kwa walivyo ukhiari uwongofu kuliko upotofu. Na siku hii basi uovu hautawagusa, wala hawatahuzunika kwa kuzikosa neema walizo kuwa wakizitaraji.

التفاسير:

external-link copy
62 : 39

ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَيۡءٖۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ وَكِيلٞ

Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya kila kitu. info

Mwenyezi Mungu Muumba kila kitu - naye peke yake - ndiye Mlinzi wa kila kitu. Anaendesha mambo yake kwa mujibu wa hikima yake.

التفاسير:

external-link copy
63 : 39

لَّهُۥ مَقَالِيدُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Yeye anazo funguo za mbingu na ardhi. Na wale walio zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kukhasiri. info

Maendesho ya mambo ya katika mbingu na ardhi yako kwa Mwenyezi Mungu. Hayaendeshi hayo isipo kuwa Yeye. Na makafiri kwa hoja za Mwenyezi Mungu na ushahidi wake ndio wao, peke yao, ndio wenye kukhasiri, mwisho wa kukhasiri! (Injili ya Mathayo 16:16-20 imedai kuwa Yesu kampa funguo za mbingu na ardhi Petro, na hivyo ndiyo Papa wa Roma amerithi funguo hizo na kuanzisha Kanisa la Kikatoliki, na uwezo wa kufutia watu dhambi na kuwaangamiza Motoni. Marcello Craveri, mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana ameandika katika kitabu chake Maisha ya Yesu (sahifa 227-28 Panther Edn.) kuwa Mathayo 16:16-20 imeongezwa na ametoa hoja 7 kwa wazo hilo. Licha ya kuwa Yesu hakumpa Petro hizo funguo za mbingu na ardhi, yeye mwenyewe Yesu hakuwa nazo.)

التفاسير:

external-link copy
64 : 39

قُلۡ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَأۡمُرُوٓنِّيٓ أَعۡبُدُ أَيُّهَا ٱلۡجَٰهِلُونَ

Sema: Je! Mnaniamrisha nimuabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu, enyi majaahili? info

Ewe Muhammad! Sema: Je! Baada ya kuweka wazi Ishara zote kuwepo Mwenyezi Mungu Mmoja wa kuabudiwa, mnaniamrisha nimuabudu mwenginewe, enyi wajinga, majaahili?

التفاسير:

external-link copy
65 : 39

وَلَقَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ لَئِنۡ أَشۡرَكۡتَ لَيَحۡبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ

Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri. info

Na ninaapa: Bila ya shaka, umepewa Wahyi, wewe, Muhammad na Mitume walio kuwa kabla yako, kwamba bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote kile basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atazibat'ilisha a'mali zako, na utakuwa katika watu walio khasirika ukomo wa kukhasiri.

التفاسير:

external-link copy
66 : 39

بَلِ ٱللَّهَ فَٱعۡبُدۡ وَكُن مِّنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Bali muabudu Mwenyezi Mungu tu, na uwe miongoni mwa wenye kushukuru. info

Ewe Mtume! Usiwakubalie kwa hayo wanayo kutaka, bali muabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na uwe katika wanao mshukuru Yeye kwa neema zake.

التفاسير:

external-link copy
67 : 39

وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦ وَٱلۡأَرۡضُ جَمِيعٗا قَبۡضَتُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَٱلسَّمَٰوَٰتُ مَطۡوِيَّٰتُۢ بِيَمِينِهِۦۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Na wala hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kadiri yake. Na Siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake, na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kuume. Subhanahu wa Taa'la Ametakasika na Ametukuka na hayo wanayo mshirikisha nayo. info

Washirikina hawakumtukuza Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki utukufu wake, wala hawakumjua kama anavyo stahiki kujuulikana, kwa kuwa wamemshirikisha pamoja naye wenginewe, na wakamtaka Mtume naye aingie katika ushirikina, na hali ardhi yote ni milki yake Siku ya Kiyama, na mbingu zitakuwa zimekunjwa, kama zinavyo kunjwa nguo, katika mkono wake wa kulia. Mwenyezi Mungu ametakasika na kila upungufu, na ametukuka vikubwa mno na vyote hivyo wanavyo mshirikisha naye.

التفاسير: