ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
6 : 39

خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ ثُمَّ جَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ ثَمَٰنِيَةَ أَزۡوَٰجٖۚ يَخۡلُقُكُمۡ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡ خَلۡقٗا مِّنۢ بَعۡدِ خَلۡقٖ فِي ظُلُمَٰتٖ ثَلَٰثٖۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُصۡرَفُونَ

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Ufalme ni wake. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi? info

Enyi watu! Mwenyezi Mungu amekuumbeni kutokana na nafsi moja, naye ni Adam, baba wa watu wote. Na amemuumba kutokana na nafsi hiyo mkewe, Hawa. Na amekuteremshieni kwa ajili ya maslaha yenu namna nane za nyama hoa, wanyama wa mifugo, madume na majike. Nao ni ngamia, na ng'ombe, na kondoo, na mbuzi. Naye anakuumbeni matumboni mwa mama zenu kwa kukua na kugeuka geuka, katika viza vitatu, navyo ni kiza cha tumbo, na tumbo la uzazi, na zalio. Huyo aliye kuneemesheni kwa neema hizi ndiye Mwenyezi Mungu, Mlezi wenu, Mwenye kumiliki mambo yenu yote. Ni Yeye tu, si mwenginewe, ndiye Mwenye utawala wa pekee. Hapana wa kuabudiwa kwa Haki ila Yeye. Basi yawaje hata wanaacha kumuabudu Yeye wakenda kuwaabudu wenginewe? Huzuka yai katika mwahala pa kufanyika mayai kwa mwanamke, hata likisha kuwa tayari hutumbukia katika mojapo ya paipu za Filopia likapita humo mpaka kufikia kwenye tumbo la uzazi Rahimi (Womb). Halifiki huko ila kupita siku kidogo, na huenda kijidudu cha manii (Sperm) ya mwanamume kikaliingia hilo yai, na hapo huanza viwango vya kugeuka na kukua kwa mwanzo. Na katika tumbo la uzazi hubaki mtoto muda wa mimba, na hujifanyia vifuniko viwili, na sehemu ya funiko moja hufanyika zalio, placenta. Na funiko jingine ndio humfunika yule mtoto khasa. Yapo maoni mbali mbali juu ya hivyo "viza vitatu" kama ilivyo tajwa katika Aya hii tukufu. Katika hayo ni Tumbo, na tumbo la uzazi, na zalio, yaani mfuko unao mfunika mtoto. (2)Tumbo la uzazi, na ile mifuniko miwili. (3) Tumbo na mgongo na tumbo la uzazi. (4) Panapo toka mayai (Mabiidh, au Ovaries), na paipu ya kupitia mayai, Fillopian tube, na tumbo la uzazi (Rahimi au Womb). Na dhaahiri ni kuwa hii ya mwisho ndiyo rai yenye nguvu zaidi, kwa sababu ni mahala patatu mbali mbali. Ama zile rai nyengine zinaonyesha kwa hakika kiza kimoja katika pahala pamoja palipo zungukwa na t'abaka kadhaa. Na Muumbaji Mtukufu ameashiria katika Kitabu chake ukweli huu wa kisayansi katika zama walipo kuwa watu hawajavumbua hayo mayai ya mwanamke na mwendo wake katika mwili ulio kuwa hauwezi kuonekana kwa macho.

التفاسير:

external-link copy
7 : 39

إِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِيٌّ عَنكُمۡۖ وَلَا يَرۡضَىٰ لِعِبَادِهِ ٱلۡكُفۡرَۖ وَإِن تَشۡكُرُواْ يَرۡضَهُ لَكُمۡۗ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُم مَّرۡجِعُكُمۡ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani. info

Enyi watu! Mkizikataa neema za Mwenyezi Mungu, basi Yeye hakika si mhitaji wa imani yenu na shukrani zenu. Lakini Yeye hapendi waja wake wakufuru, kwa sababu hayo yanawadhuru wenyewe. Na mkimshukuru kwa ajili ya neema zake, Yeye huwa radhi nanyi kwa shukra hiyo. Wala mtu mwenye madhambi hayabebi madhambi ya mwenginewe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, na hapo atakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda duniani. Hakika Yeye anayajua mnayo yaficha katika nyoyo zenu ziliomo vifuani. Haya yaliomo katika Qur'ani Tukufu yanaweka wazi msingi wa kutoa adhabu, kama ilivyo vile vile katika Surat Yusuf katika kauli yake Mtukufu: "Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali sisi kumshika yeyote ila tuliye yakuta mali yetu kwake; hivyo basi tutakuwa madhaalimu." Na haya katika Qur'ani ni kusimamisha msingi ulio kwisha tajwa, nao ni msingi ambao haukuthibiti katika kanuni (sharia) za kutungwa na binaadamu ila katika zama za karibuni. (Haya ni kinyume cha ilivyo katika imani aliyo itumbukiza Paulo katika Ukristo, kwamba wanaadamu wamerithi dhambi ya Adam, wanayo ita "Dhambi ya asili", na kwamba Nabii Isa, Yesu, kafa msalabani kwa kubeba dhambi za wanaadamu. Biblia yenyewe inapinga haya. Tazama: Jeremiah 31:29-30; Ezekieli 18 Kwa nadhariya ya Paulo Mungu amedhulumu mara mbili: 1. Kutubandika wanaadamu wote dhambi za Adam, 2. Kumbebesha "mwanawe" Yesu dhambi za walimwengu wote!)

التفاسير:

external-link copy
8 : 39

۞ وَإِذَا مَسَّ ٱلۡإِنسَٰنَ ضُرّٞ دَعَا رَبَّهُۥ مُنِيبًا إِلَيۡهِ ثُمَّ إِذَا خَوَّلَهُۥ نِعۡمَةٗ مِّنۡهُ نَسِيَ مَا كَانَ يَدۡعُوٓاْ إِلَيۡهِ مِن قَبۡلُ وَجَعَلَ لِلَّهِ أَندَادٗا لِّيُضِلَّ عَن سَبِيلِهِۦۚ قُلۡ تَمَتَّعۡ بِكُفۡرِكَ قَلِيلًا إِنَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِ

Na taabu inapo mfikia mtu humwomba Mola wake Mlezi naye ameelekea kwake. Kisha akimpa neema kutoka kwake, husahau yale aliyo kuwa akimwitia zamani, na akamfanyia Mwenyezi Mungu washirika ili apoteze watu njia yake. Sema: Starehe na ukafiri wako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. info

Na mtu akifikiwa na shida yoyote katika shida za dunia humwomba Mola wake Mlezi, na hurejea kwake, baada ya kuwa akimpuuza. Kisha Mola wake Mlezi akimpa neema kubwa husahau zile taabu alizo kuwa akimwombea Mola wake Mlezi amwondolee na amfarijie kabla hajamneemesha kwa neema hizo. Na humfanyia Mwenyezi Mungu miungu washirika walio sawa na Yeye kwa kuwaabudu. Huyo mtu hufanya haya ili ajipoteze yeye na wenginewe waiache Njia ya Mwenyezi Mungu. Ewe Muhammad! Mwambie huyo mwenye sifa hizi kwa kumwonya: Starehe na huko kuzikanya kwako neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yako kwa muda mchache. Kwani hakika wewe ni katika watu wa Motoni.

التفاسير:

external-link copy
9 : 39

أَمَّنۡ هُوَ قَٰنِتٌ ءَانَآءَ ٱلَّيۡلِ سَاجِدٗا وَقَآئِمٗا يَحۡذَرُ ٱلۡأٓخِرَةَ وَيَرۡجُواْ رَحۡمَةَ رَبِّهِۦۗ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُونَ وَٱلَّذِينَ لَا يَعۡلَمُونَۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ

Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji rehema za Mola wake MleziSema: Ati watakuwa sawa wale wanao jua na wale wasio jua? Hakika wanao kumbuka ni watu wenye akili. info

Je! Mwenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu nyakati za usiku anao upitisha na hali yeye yumo kusujudu na kusimama, akiiogopa Akhera, naye anataraji rehema ya Mola wake Mlezi, ni kama anaye mwomba Mola wake Mlezi wakati wa shida na akamsahau wakati wa neema? Ewe Muhammad! Waambie: Ati wanakuwa sawa wenye kujua haki za Mwenyezi Mungu wakamuabudu Yeye tu peke yake, na wale wasio jua wakapuuza kuziangalia Ishara? Hakika wenye akili nzuri ndio wanao waidhika.

التفاسير:

external-link copy
10 : 39

قُلۡ يَٰعِبَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمۡۚ لِلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٞۗ وَأَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٌۗ إِنَّمَا يُوَفَّى ٱلصَّٰبِرُونَ أَجۡرَهُم بِغَيۡرِ حِسَابٖ

Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu. info

Ewe Nabii! Sema kwa kufikisha Ujumbe unao toka kwa Mola wako Mlezi: Enyi waja wangu mlio niamini! Jikingeni na ghadhabu za Mola wenu Mlezi. Mwenye kutenda mema atalipwa mema, duniani kwa kusaidiwa, na Akhera kwa Pepo. Wala msikae katika unyonge, kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu ina wasaa. Na subirini kwa kufarikiana na nchi zenu na wapenzi wenu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu huwalipa wenye kusubiri ujira wao mara zisio ingia katika hisabu za wanao hisabu.

التفاسير: